JAMII YATAKIWA KUACHA ANASA
JAMII nchini imeaswa
kuachana na uchangiaji wa anasa badala yake ijikite zaidi kuyajali makundi yasiyojiweza hususani
watoto yatima na wenye maambukizi ya ukimwi wanaolelewa bila msaada wa uhakika kwenye
vituo vya watoto yatima .
Hayo yalisemwa jana na
mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano cha jijini Arusha,Godiliste Temba wakati
kikundi hicho kilipotembelea na kutoa msaada wa vyakula na vinywaji kwa vituo
viwili vya kulelea watoto yatima kikiwemo
kituo Sant Lusia kilichopo Moshono jijini Arusha ,kinacholea watoto wenye
maambukizi ya ukimwi pekee na kituo cha Sant
Joseph kilichopo kata ya Mlangalini wilayani Arumeru.
Temba aliwaomba watanzania kujijengea utaratibu wa kujisaidia
wenyewe na kuachana na dhana iliyojijenga ya kutegemea wafadhili pekee kutoka nje ya nchi ambao wengi wao wamekuwa wababaishaji huku wakiweka
masharti magumu na misaada yao .
Aidha alisema jamii inakila sababu ya kuguswa na tabu
wanayoipata watoto yatima kwani mbali na kukabiliwa na changamoto nyingi
kimaisha wamekosa msaada muhimu ya kijikimu hususani elimu bora itakayowasaidia
kuondokana na utegemezi hapo baadae.
Ametoa rai kwa kila
mtanzania kwamba jukumu la kuyasaidia makundi hayo ni wajibu wakila mtu iwapo ataguswa nakujitolewa walau kuchangia
mtoto mmoja kila mwaka ikiwepo kumsombesha na kuachana na uchangiaji mkubwa wa anasa ambao
umekuwa ukipoteza fedha nyingi kwa muda mfupi.
‘’suala la kuwasaidia
watoto ni jukumu la kila mtu ni vizuri basi kwa kila mtanzania iwapo ataguswa
kwa namna yake na kutoa mchango kwani wengi wetu tumekuwa tukijitoa sana kuchangia
harusi zakifahari,bila kujali kuwa michango yetu pia inahitajika kwa makundi
mengine muhimu’’alisema
Naye Mkuu wa kituo cha
watoto yatoma cha St.Lucia Winfrida Mrema,alisema kuwa kituo chake kinalea watoto
wenye umri wa miaka 2 hadi 10 wenye maambukizi ya VVU na kimekuwa kikikabiliwa
na changamoto kubwa ya upungufu wa lishe
bora kwa watoto hao.
Aliwaomba wananchi
kuendelea kujitolea kuwasaidia watoto hao kwani wengi wao hawana wazazi na
wamekuwa wakiletwa kituoni hapo wakiwa kwenye hali mbaya ya maambukizi ya
ukimwi baada ya kutelekezwa na wazazi
wao au baadhi wazazi kufariki dunia na kuwaacha yatima bila msaada .
Aidha kwa upande wa
mmiliki wa kituo cha St.Joseph Sister Crispin Mnate.. alisema kuwa kituo hicho kina
jumla ya watoto yatima 46 na wamekuwa wakilelewa katika mazingira magumu
kutokana na kukosa ufadhili wa kudumu.
Alisema changamoto
kubwa inayokikabili kituo hicho ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuwalipia ada wanafunzi wanaosoma ndani na nje ya jiji la
Arusha chini ya uangalizi wa kituo hicho wakiwemo wawili wanaosoma shule za sekondari.
Alisema amekuwa akipokea watoto wachanga wanaozaliwa na wazazi
wao kisha kutelekezwa ama kutupwa majalalani na kuwaanzishia huduma ya matunzo
hadi kufikia umri mkubwa ,hivyo alidai kuwa uwezo wa kumudu kuwahudumia watoto
hao ni mdogo na kuwataka watu binafsi ,mashirika ya umma na taasisi mbalimbali
kujitokeza kusaidia vituo hivyo vya
kulelea watoto yatima.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia