Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE AJIPANGA KUWAINUA WANANCHI WA JIMBO LAKE


Mbunge wa  Jimbo la Kondoa  Kusini Juma Nkamia amedhamiria kuwainua kiuchumi  wananchi wa jimbo hilo kwa kutoa zaidi ya milioni 65 kwa ajili ya kusaidia vikundi  kupata mitaji kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo ili  kukabiliana na tatizo gumu la ukosefu wa ajira hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ziara yake  jimboni humo Nkamia alisema kuwa kiongozi wa kweli ni lazima awatumikie wananchi wake kwa kuwapunguzia makali ya maisha ikiwa ni pamoja na kutimiza ahadi mbalimbali ambazo aliwaahidi wananchi kipindi cha kampeni.

Ameeleza kuwa fedha hizo zitasaidia kuinua vikundi vya vijana na akina mama ili waweze kupata mitaji kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali itakayowasaidia kuinua uchumi wao na kuweza kuendesha familia zao.

“hizi milioni 65 ni mitaji katika vikundi vya akina mama na vijana kila kata ili waweze kupata mitaji ya kuendesha miradi mbalimbali ili waweze kupata kipato ambacho kitasaidia kuinua uchumi wa wananchi na hatimaye uchumi wa jimbo.”alisema Nkamia

Akiwa katika kata ya Paranga ambako alikabidhi zaidi ya shilingi milioni tano katika kata hiyo kwa vikundi vya kina mama na taasisi za kidini, Nkamia alilamikiwa na mamia ya wananchi alisema lengo kubwa ni kuendeleza vijana na akina mama ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi ili wasiwe tegemezi.

Mbunge huyo kijana akizungumza katika kadhaa ya ziara zake za kikazi jimboni humo alimshukuru rais Jakaya Kikwete kwa kuigawa wilaya ya Kondoa na kuanzisha wilaya mpya ya Chemba ambayo ndio jimbo la Kondoa Kusini kwa jinsi anavyowajali wananchi wa wilaya hiyo akisema hiyo itasaidia kuharakaisha maendeleo ya wilaya hiyo mpya ambayo itakuwa na mamlaka kamili ya baraza la madiwani baada ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Wilaya  hiyo mpya ya Chemba ina kata ishirini na na vijiji zaidi ya ishirini na vitatu 

Mbunge huyo wa Kondoa Kusini amewataka vijana kutodanganywa na vyama vya upinzani ambavyo vinawalaghai kuwa vitawapatia kila kitu bure kitu ambacho amesema hakijawahi kutokea duniani kote.

“nimekakaa katika nchi kubwa duniani marekani na Uingereza zaidi ya miaka sita sijaona nchi yoyote duniani ambayo vijana wanagawiwa pesa na chama cha siasa zadi ya kila chama chenye dola kuweka mikakati ya kuwainua kiuchumi kwa kuwajengea mitaji ya kujiimarisha kiuchumi”alisema  Nkamia.

Akizungumzia baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa majuzi na Rais Kikwete  Nkamia amesema rais amezingatia maeneo ya nchi na amewachanganya wazee na vijana na katika baraza hilo ambalo anaamini litafanya kazi vizuri kwa manufaa ya watanzania wa kada zote na amempongeza rais kwa kuzingatia mawazo ya wabunge ambalo lilionyesha udhaifu wa baadhi ya mawaziri katika ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za seruikali CAG.

Akijibu hoja za wananchi ambao walimuuliza kwa nini Rais hakumteua yeye au mbunge mwenzake wa Kondoa Kusini  Nkamia alisema rais ameujali mkoa wa Dodoma kwa kuongeza naibu waziri mmoja katika baraza hilo na kuwa ni faraja kwa wananchi wa mkoa huo ambao uliongoza kwa kitaifa kwa kuipatia ccm kura katika uchaguzi uliopia na akaongeza kuwa bunge lina wabunge zaidi ya mia moja na themanini wa ccm na nafasi za uwaziri si zaidi ya thelathini na ni vigumu kwa rais kumteua kila mtu lakini akawataka wananhi kuendelea luicgagua ccm na wala wasivunjike moyo kisa wabunge wao hawakuteuliwa kuwa mawaziri.

Mbunge huyo amesema wananchi wamewachagua wabunge hawakuchagua mawaziri na mwene mamlaka ya mwisho kuteua mawaziri ni rais na itakuwa si busara kwa wananchi au baadhi ya wabunge kumlaumu rais kwa kutowateua katika baraza la mawaziri.

Habari na mdau wa libeneke Ashura  mohamed aliyekuwa kondoa

Post a Comment

0 Comments