WATUMISHI wa kata ya Naisinyai Wilaya ya
Simnjiro Mkoani Manyara wameanzisha mfuko wakujikimu wenye
shilingi 840,000 utakaowasaidia kwenye shughuli zao za maendeleo na wakiwa
matatizoni.
Wakizungumza mbele ya Diwani wa
kata hiyo,Kilempu Ole Kinoka watumishi hao walidai kuwa mfuko huo utakuwa
endelevu na utawasaidia watumishi wakiwa katika matatizo yoyote yatakayojitoka
ghafla.
Walisema wameazimia kila siku ya
jumamosi ya kwanza ya mwezi wawe wanakutana na kuchangia asilimia fulani ya
mishahara yao kwa ajili ya kuwapunguzia ukali wa maisha uliopo hivi sasa sehemu
tofauti hapa nchini.
Akizungumza na watumishi hao Diwani
wa kata ya Naisinyai,Kilempu Ole Kinoka aliwapongeza kwa kuanzisha mfuko huo
ambao utakuwa unawakimu na kuwawezesha pindi watakapokuwa wamekwazika mahali
fulani.
Pia Ole Kinoka alikubali kuwa mlezi
wa mfuko wa kikundi hicho cha watumishi wa kata hiyo na kudai kuwa atakuwa
pamoja nao katika kuendeleza mfuko huo ambao utakuwa na manufaa kwao.
Aliwataka watumishi hao kuongeza
juhudi katika kuitumikia jamii ya eneo hilo kuliko kung’ang’ania kuboreshewa
maslahi yao huku utendaji kazi ukiwa duni na wananchi
wanawalalamikia.
Alisema kuwa watumishi wa kata hiyo
wakiweka mbele uwajibikaji na utendaji kazi mbele ya jamii hata yeye atakuwa
mstari wa mbele katika kutetea maslahi yao kwenye halmashauri ya wilaya
hiyo.
Habari imeandikwa mdau wa libeneke Qeen Lema ,Arusha
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia