MTU mmoja aliyetambukika kwa jina Israe Ngonda(45) mkazi
wa kijenge juu jiijini Arusha ameuawa kwa kuchinjwa kama kuku na kitu chenye
ncha kali na watu wasiojulikana nyumbani kwake na mwili wake kuachwa kitandani
akiwa amepiga magoti na kichwa kulalia kitandani.
Kwa muijbu wa kamanda wa polisi mkoani Arusha,ACP
Liberatus Sabas ,mwili wa marehemu ulikutwa majira ya asubuhi baada ya majirani
kupita eneo hilo na kukuta mlango wa marehemu ukiwa wazi ndipo walipojaribu
kuingia ndani huku wakimwita jina lake bila kuitikiwa.
Alisema polisi walipata taarifa na kufika eneo la tukio
ambapo walimkuta marehemu huyo akiwa amepiga magoti huku sehemu kubwa ya mwili
ukiwa umelazwa kitandani na sehemu ya shingo yeke ikiwa imekatwa na kitu chenye ncha kali.
Aidha Sabas aliongeza kuwa hakuna mtu yoyote
anayeshikiliwa hadi sasa kuhusiana na tukio hilo na polisi wameanzisha
uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Hata hivyo taarifa zaidi kutoka kwa mashuhuda
wa tukio hilo wamebainisha kuwa kabla ya tukio hilo marehemu alichomewa nyumba
yake na watu wasiojulikana na baadae wanakijiji walifanikiwa kuuzima moto huo.
Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa akiishi pekee baada ya
familia yake kusafiri na kwamba tukio hilo linahusishwa na ulipizaji wa visasi.
Tukio kama hilo liliwahi kutokea hivi karibuni wilayani
Arumeru,baada ya mwenyekiti wa chadema ,kata ya Usariver ,Msafiri Mbwambo kuuawa
kwa kuchinjwa na watu wasiojulika.
Katika tukio jingine, mkazi wa kwa Mrombo jijini Arusha aliyefahamika kwa jina la Maswi
Marema (45) amefariki dunia baada ya
kupigwa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za uporaji.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, ACP Liberatus Sabas
alisema kuwa, tukio hilo limetokea mei 23 mwak a huu majira ya saa 3;00 asubuhi
katika eneo la Ilboru katika halmashauri ya Arusha.
Alifafanua kuwa marehemu akiwa na wenzake wasiojulikana
katika eneo la Raskazone Sakina wakitumia usafiri wa pikipiki aina ya Toyo
yenya namba T 192 BVP walikwenda katika duka la kuuzia vifaa vya shule na
Vocha na kujifanya wanahitaji huduma ya
Vocha.
Alisema mhudumu wa duka hilo aliyetambulika kwa jina la
Janet Erick (25)aliinama kwa ajili ya kuwatolea vicha ya shilingi 1000,lakini
mara baada ya mhudumu huyo kuinama walimnyooshea bastola na kumtaka awapatie
fedha za mauzo,hali iliyomlazimu kutoa kiasi cha shilingi 2,300,000.
Baadae walimwamuru mteja Amani Joseph aliyekuwa dukani
hapo akinunua mahitaji ,atoe alichonacho,ambapo walimpora fedha tasilim shilingi 210,000 na simu ya mkononi aina ya
Sumsun yenye thamani ya shilingi 108,000 na kutokomea kusikojulikana.
Aliongeza kuwa mteja aliyeporwa na watu hao aliamua
kuchukua pikipiki nyingine na kuwafuatilia na walipofika eneo la Triple
A,majambazi hao walipata ajali kwa kugongana na pikipiki nyingine .
Ambapo
aliomba msaada kwa wananchi na askari wengine kwa kuwaeleza kuwa watu hao
walikuwa majambazi waliokuwa wamewapora,ndipo kundi la watu walipoanza kumshambulia
jambazi marehemu huyo huku jambazi
mwingine akifanikiwa kutoroka.
Alisema jambazi huyo alifariki dunia wakati akipelekwa
katika hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu.
Wakati huo huo,mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la
Jovis Tarimo (37)amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa akisafiria kuacha
njia na kukonga kingo za daraja eneo la Iliboru ,jijini Arusha.
Kamanda Sabas alisema marehemu alikuwa akitumia pikipiki
aina ya Skygo yenye namba za usajiri T 972 BUM ,akitokea eneo la Sanawari
kuelekea Mianzini majira ya saa mbili na
Robo Usiku.
Miiili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya
Mkoa Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi zaidia wa jeshi la polisi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia