BREAKING NEWS

Sunday, May 20, 2012

WANANCHI 4000 WAMSINDIKIZA NASSARI KUTOA SADAKA YA SHUKRANI



 Mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye inasemekana pia ni daktari wa hospitali ya KCMC akifurahisha waumini na pambio
 wakiimba pambio
 Nassari akitoa neno la shukrani
 Nassari akiweka sadaka yake ya shukrani hivi leo
  mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki akiwa namasindikiza mjane wa marehemu kiriro ambaye alikuwa mmeru wa kwanza kwenda kudai uhuru  akimpeleka kutoa sadaka shukrani mara baada ya kuchaguliwa kuwa mmbunge

 wabunge hao wakiwa wamesimama kabla ya kuombewa katika kanisa la FPCT Kalinga hivi leo
wachungaji wakiwa wanawaombea wabunge hao
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida jana Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari aliwakutanisha wapiga kura wake zaidi ya 4000 huku miongoni mwao wakiwa ni makada wa chama cha Mapinduzi pamoja huku Mgombea mwenza wa chama cha Mapinduzi Bw Sioi Sumari akishindwa kufika kwa kuwa amekosa usafiri wa haraka sana.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mbunge huyo kutoa sadaka mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo  ibada ambayo ilifanyika katika kanisa la FPCT Kilinga wilayani Meru Mkoani Arusha

Akiongea na Maelfu ya wananchi wa jimbo hilo katika kanisa hilo Bw Nassari alisema kuwa ameamua kutoa sadaka maalumu ya kushukuru mungu mara baada ya kumaliza vema uchaguzi huku wapiga kura wake wote wakiwa salama tofauti na pale ambapo wengi waliadhimia

Pia alisema kuwa kwa sasa Viongozi wa Vyama vingine ambao nao walishiriki katika uchaguzi hawapswi kukataana na badala yake wantakiwa kuwa wamoja kama walivyoshirriki makada wengine wa chama cha Mapinduzi ndani ya ibada hiyo ya shukurani

“leo nimetoa shukurani yangu ndani ya kanisa hili la Kilinga lakini ninafurai kuwa makada wa CCM tupo nao hapa lakini mbali na hayo mgombea wangu mwenza wakati wa kampeni naye alikuwa anatamani sana kuja ila kwa bahati mbaya alichelewa ndege , ingawaje kwa sasa tuna madiwani wengi sana wa CCM,  Mbunge wa Jimbo la Moibara na wengine wengi nah ii ndio inayotakiwa”alisema Bw Nassari

Awali aliongeza kuwa yeye hana shida yoyote na kiongozi hata kama ni wa chama chake ila ana shida na viongozi ambao wana mikakati na malengo mbalimbali ya kuteketeza  maslahi ya wananchi hasa wa jimbo la Arumeru Mashariki na kamwe kiongozi kama huyo hataweza kumvumilia  kwa kuwa hana msimamo na Taifa

Naye Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye ni Mbunge wa  Mwibara mkoani Mara, bw Kingi Lugora alisema kuwa ili kukabiliana na hali zote ndani ya nchi wapo baadhi ya viongozi ambao wanaharibu mpango wa Mungu hasa kwa nyakati za uchaguzi kwa kuwa wanatumia mabavu ya Rushwa na mara wanapopata uongozi bado wanaendeleza hali ya Rushwa  huku wananchi wa chini nao wakiwa wanazidi kuumia na hali ngumu ya maisha

“wapo wanasiasa ambao wanawapiga wananchi upofu wa Rushwa na ndio maaana uchumi wa leo umeyumba huku waumini wa leo wakiwa wanasuasua na kwa hili naomba makanisa ya sasa yaingie kwenye  maombi dhidi ya hawa watu ambao wanaomba rushwa hasa katika bunge, na pia napenda kuwatia Moyo hata wabunge ambao  wanajidhatiti na kisha kusema hadharani masuala ya Rushwa wasiogope hata kama ni makada kama mimi nilivyo  kwa kuwa wapo baadhi ya viongozi  ambao wanatamani kusema Rushwa lakini wanapata Kigugumizi kwa kuhofia maslahi ya vyama vyao”aliongeza Bw Lugora.

Pia alisema kuwa yeye kama yeye kamwwe hatasita kusema ukweli kwa kada yoyote  wa CCM  ambaye anachangia sana  uchumi wa Nchi kuyumba na badala yake atamuomba Mungu zaidi  ili aweze  kuwasema na kuwaweka hadharani kwa kuwa mpaka sasa Mungu anajibu Maombi juu ya mafisadi  ambao ndio chanzo kikubwa sana  cha umaskini ndani ya Nchi ya Tanzania


Katika hatua nyingine  Askofu Langaeli  Kahaya  naye alisema kuwa wananchi wanapswa kuhakikisha kuwa kamwe hawamchagui kiongozi yoyote kwa ajili ya maslahi ya Rushwa kwa kuwa wote wanaotoa rushwa  ndio wanaosababisha hata umaskini na umwagaji damu ndani ya  nchi

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni mwiko kwa wananchi wma Jimbo la Arumeru  Mashariki kujihusisha na Rushwa kwa vipindi vyote vya uchaguzi kwa kuwa mpaka sasa Rushwa imeshaacha madhara makubwa sana ndani ya jimbo hilo na pia Rushwa ni dhambi kubwa sana.

“ukiangalia sana mtu anayetoa rushwa ni mtu mwenye elimu yake sasa kwa hili wananchi wanapswa kujua kuwa anayetoa na anayepokea rushwa anafanya dhambi na hiyo dhambi ndiyo inayotapakaa kwa jamii na vizazi vingine ambavyo navyo vinaibuka na  dhambi hiyohiyo”alisema Bw Kaaya

Mbali na hayo alisema kuwa pia taifa la Tanzania linatakiwa kuhakikisha kuwa kila mara linakuwa na maombi makubwa sana hasa ya baadhi ya watu ambao wanatekeleza  ahadi za Rushwa na Ufisadi hali ambayo nayo inachangia ka kiwango kikubwa sana umaskini wa watanzania wa Leo

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates