WANAFUNZI watatu walioitimu mafunzo ya kompyuta katika chuocha uhifadhi wa mazingira cha University Times training Insititutekilichoko moivaro mkoani hapa wamepatiwa kompyuta tatu zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili ikiwa ni njia ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe baada ya kuhitimu mafunzo yao.
Wanafunzi hao wamekabidhiwa kompyuta
hizo na mkurugenzi wa chuo hicho bw Solomon Njiamoja alipokuwa
katika hafla ya mahafali ya kwanza ya
wahitimu wa hoteli management na kompyuta
yaliyofanyika chuoni hapo.
Njiamoja alisema kuwa chuo hicho
kimeamua kuwapa wanafunzi hao kompyuta hizo ili ziweze kuwasaidia
katika kujiajiri wenyewe ambapo wataweza kukabiliana na hali ngumu
ya kimaisha kwa kuwa vijana wengi wanashindwa kutimiza malengo yao kwa ajli ya
kukosa vitendea kazi.
Aidha aliongeza kuwa ili kuhakikisha
kuwa wanafunzi wanahohitimu chuoni hapo wanapata mafanikio mazuri chuo hicho
kinatarajia kutoa kompyuta 105 kwa mwaka ambapo kila mwanafunzi anayefanya
vizuri katika somo hilo atapata kompyuta yake ya kumuwezesha
kujiajiri.
Mkurugenzi huyo akielezea malengo ya
chuo hicho alisema kuwa kinatarajia kuanzisha redio pia kuanzisha mfuko maalum
wa kuendeleza waalimu kwa kuwa walioko wana shahada ya kwanza hivyo
haiwatoshelezi kutoa elimu .
Awali mgeni rasmi katika mahafali
hayo diwani wa kata ya sokoni one Maiko Kivuyo aliwataka wanafunzi
hao kutumia kompyuta hizo vizuri kwa kuzitunza na
badala yake wasiziuze kwani wako baadhi ya vijana wakipewa zawadi
wanakimbilia kuuza ili wapate fedha.
Aliwataka vijana hao kutumia elimu hiyo
waliyoipata vizuri kwa kuwa katika dunia ya sasa hakuna kitu
unachoweza kufanya bila kutumia kompyuta.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia