Jeshi la polisi mkoani hapa limewafikisha watu saba
mahakamani kufuatia na kuhusika na matukio matatu tofauti yakiwemo ya mauaji yaliyotokea wilayani Arumeru mkoani hapa.
Tukio la kwanza ambalo lilitokea ni la mauaji ya mwenyekiti
wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema wa kata ya usa river aliyejulikana kwa jina la Msafiri Mbwambo
(32) mkazi wa magadini yaliyotokea Aprili 27 majira ya saa 2:00 usiku na saa 3:00
usiku katika eneo la mji mwemea na tukio
la pili ni la mauaji ya Martha Josephy (75)makazi wa nkorenkoli wilayani arumeru huku tukio la tatu ni la
kusababisha kifo cha Noel eliona (25) mkazi wa sing’isi wialyani humu
kilichotokea april 28 majira ya saa 4:30 usiku baada ya yeye na wenzake kuvamia
shamba liitwalo mito miwili mali ya Agha Khan University ambalo kwa sasa
limekodishwa kwa Rekesh Vohala.
Akiongelea matukio haya yote Naibu kamishna wa polisi Isaya Mngulu alisema kuwa kutokana na matukio hayo
jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa 12 na kuwahoji na mpaka sasa watuhumiwa saba wamefikishwa mahakamani huku watuhumiwa
wengine watano wakiwa wanahojiwa.
Alibainisha kuwa
uchunguzi ulifanywa na na jeshi
la polisi mkoani hapa umebainisha kuwa matukio hayo yametokana na sababu
mbalimbali na si kama baadhi ya watu wanavyodai kuwa yanatokana na siasa huku
akitolea mfano tukio la mauaji ya Martha Joseph
ambaye alifariki nkorenkoli
wilayani arumeru tukio ambalo lilitokana
na imani za kisherikina ambapo baadhi ya wanachi walikwenda nyumbani kwa
marehemuy na kumchukua na kumpeleka kwenye kiwanja cha shule mojawapo iliyopo
karibu na eneo hilo kasha kuuwa kwa kumpiga mawe na kuuchoma mwili wake moto.
“kutokana na tukio hilo tu la mtu huyu jeshi la polisi
tayari limemkamata mtu mmoja aitwaye Charles Isawafu Nko maarufu kwa jina la
Mwarabu ambaye amefikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tukio hili la mauhaji
,mbali na hilo pia tumewakamata watu wengine watatu ambao waliusika na mahuaji
hayo na katika uchunguzi ambao tumeufanya jeshi la polisi limebaini kuwa
marehemu msafiri alikuwa na mzozo na baadhi ya viongozi wa vitongoji kutonkana
na kuwa msari wa mbele katika ufatiliaji
mapato na matumizi ya miradi mbalimbali nani ya kata hiyo na pia alikuwa maarfu
sana hivyo kuwa tishio kubwa hasa kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa,hali
iliyofanya baadhi ya viongozi hao
kumchukia na hatimaye kupanga njama za kuua.
Aidha alisema kuwa waliofikishwa mahakamani kutokana na
tukio hili ni Daudi Lezele Mkumba
,Mathaias Nathan Kurwa pamoja na Said Mkwela huku akibainisha kuwa katika tukio
la tatu ambalo lilihusiana na shamba lililojulikana kwa jina la mito miweili
watu zadi ya ishini walivamia shamba hilo na kuvunja stoo kasha kuiba mbolea na
mbegu mbalimbali za mazao na kasha kuchoma moto stoo hiyo iliyokuwa na materkta
,jenereta la kufa umeme na kusbanisha hasara ya shilingi Tshs 222,775,000/=
milioni mia mbili na ishirini na mbili laki saba na elfu sabini na tano na katika tukio hilo mmoja wa wavamizi hao
aliyejulikana kw ajina la Noel Eliona alikutwa amefariki huku akiwa na jeraha
kichwani ambalo lilitokana na mapambano kati yao na askari ambalo walikuwa
wanahami enehilo lisivamiwe .
Alibainisha kuwa kufuatia tukio hilo jeshi la polisi linawashilillia watuhumiwa watatu
ambao ni Godlove Salael(26)mkulima mkazi wa sing’si,Anthony Piniel kiungai(23)mkulima pamoja na Judiac Abrahamu kitomary (26)ambaye
ni dereva ambapo alisema watuhumiwa wote hawa wamefikishwa mahakamani leo
(jana) kwa kosa la kuharibu mali .
“sasa napenda kusema kuwa matukio hayo yote yamefanya idadi
ya watuhumiwa saba kufikishwa mahakamani huku wengine watano bado tunawahoji na
upelelezi utakapo kamilika tutawapa taarifa ila napenda kusema kuwa toka tarehe
1 mwezi huu kumekuwa na taarfa ya viongozi wa kisiasa kutumiwa ujumbe wa
vitisho lakini uchunguzi wa awali wa jeshi letu umebaini kuwa watu hao
walijitumia ujumbe huo wenyewe kwani hata mmiliki wa namba inayotuma ujumbe huo
kwa wengine unaonyesha kwamba hata yeye mwenyewe amejitumia kwenye namba yake
ingine ivyo napenda kuwaambia viongozi wasipende kucheza na jeshi la polisi na
sisi tunahakili na tunajua kila kitu”alisema Mngulu
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia