BREAKING NEWS

Wednesday, May 16, 2012

TAMASHA LA VYOMBO WA HABARI KUFANYIKA JULAI MOSI

TAMASHA la saba la vyombo vya babari Kanda ya Kaskazini, linatarajiwa kufanyika Julai mosi, mwaka huu katika viwanja vya General Tyre mjini hapa.

Katibu wa  chama cha Waandishi wa habari za michezo na Burudani mkoani Arusha(TASWA Arusha) Mussa Juma alisema  Tamasha hilo mwaka huu, linatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.

Alisema  katika tamasha hilo, ambalo uratibiwa na kampuni ya Ms Unique Promotion , litashirikisha  wanahabari wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, pamoja na  Dar es Salaam.

Alisema  timu nyingine ambazo zinatarajiwa kushiriki ni TBL Arusha, PEPSI,CRDB, NMB,Wazee Klabu, Kitambi Noma,Vodacom, Exim Bank,NSSF Arusha na nyingine kadhaa.

"mwaka huu tunatarajia mchuano utakuwa ni mkali hasa katika soka ambapo bingwa mtetezi ni Radio 5"alisema Juma. 

Alisema kabla ya tamasha kutakuwa na semina ya wanahabari wa michezo kanda ya kaskazini.

Hata hivyo, alisema bado chama hicho, kinafanya mazungumzo na wadhamini mbali mbali ni kufanikisha tamasha hilo la kila mwaka.
Wakati huo huo,Chama cha waandishi wa habari na michezo mkoa wa Arusha(TASWA- ARUSHA), kimetoa salamu za pole  kwa familia ya aliyekuwa, Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Mtanzaia   Rachel Mwiligwa ambaye amefariki mwishoni mwa wiki na kuzikwa.

Katika taarifa ya TASWA Arusha kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Katibu wake, Mussa Juma, juzi alisema kifo cha Rachel    ni pigo kwa familia yake, wanahabari na gazeti la Mtanzania
.

"sisi kama TASWA Arusha tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwanahabari mwenzetu Rachael ambaye alikuwa nguli katika masuala ya michezo"alisema Juma

Rachael alikumbwa na umauti usiku wa kuamkia ijumaa kwenye hospitali ya Mwananyara Jijini Dar  na amezikwa juzi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates