ABIRIA WATESEKA USAFIRI ARUSHA
Wananchi wa mkoani Arusha leo wamepata tabu sana ya kusafiri kutokana na mabasi
yaliyokuwa yanafanya safari zake za kwenda
mkoani Kilimanjaro kugoma kutokana na madai kuwa ushuru wa standi
kupanda
Libeneke la kaskazini lilishughudia wananchi hao ambao wengi wao
walikuwa wanaelekea katika sehemu zao za kazi huko mkoani Kilimanjaro wakipata
shida ya kupata mabasi huku wengine wakilazimika kulipa nauli
kubwa ili mradi tu wafike wanapoenda.
Wakiongea kwa nyakati tofauti abiria hao walikuwepo standi
hapo ambapo mmoja wapo alijitaja kwa jina la Msafiri jamali yeye alisema kuwa
kugoma huko kwa mabasi kumewaletea matatizo makubwa kwani wengine walikuwa
wanaenda mkoani Kilimanjaro katika kazi huku akisema kuwa mbali na mabasi ya
fanyayosafari ya moshi kugoma (kosta) pia magari makubwa ambayo yanapita katika
mji huo yamekuwa yakitaka nauli sawa na mtu ambaye anaenda dar.
“mbali na magari kukosekana lakini pia kuna magari
yanayoenda dar yanapita apo hapo moshi lakini yanataka ukipanda basi hilo basi ulipe nauli kabisa ya dar kama ni 250000 ulipe
ili wakufikishe moshi kitu ambacho wanatuumiza sana sisi wasafiri jamani”alisema Elifuraha
kileo.
Kutokana na matatizo hayo libeneke lilibisha hodi kwa kamanda wa
kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha Arson Mwakyoma azunguzie swala hilo naye alisema kuwa ni
kwali swala hilo lipo ila wapo katika mazungumzo na mdua sio mrefu watatoa jibu
sahihi .
Alisema kuwa yeye anaamini kuwa magari ya mkoani Arusha
hayajagoma bali yanaogopa kwenda mkoani Kilimanjaro na abiria kwani wakienda
wanaweza kufanyiwa fujo na wenzao wa
mkoani huko waliogoma .
Alibainisha kuwa tatizo hili lipo na linasemekana ni
kutokana na halimashauri ya manispaa ya mkoa wa Kilimanjaro kupandisha bei za kulipia ushuru wa mabasi standi pasipo
ya kuwashirikiksha wamiliki wa mabasi ,pamoja na madereva na makondakta.
Alisema kuwa anasikitishwa sana
na watu hao ambao wanawazuia wenzao na wao kama
jeshi la polisi wameamua kuwachukulia hatua kali wale wote ambao watabainika
wanawaletea fujo madereva ambao watakuwa wanawasafirisha abiria .
Kwakweli ni kitu kinachosikitisha kuona mtu ambaye analipa
ushuru anagoma kubeba abiria kwakweli inasikitisha na wewe mwenyegari kumbuka
unavyoweka gari yako pasipo kubeba watu basi unajikomoa mwenyewe maaana kama ni
ushuru upo pale pale na utaulipa tu hivyo kama
kunatatizo ni bora magari yafanye kazi huku mazungumzo yakiendelea kuliko
kugoma na kuwatesa wananchi
“mimi naona cha muhimu ni kukaa mezani na kutafuta suluhu
kuliko kufanya haya mambo ambayo wanayafanya kwakweli “alisema Mwakyoma
|Naye katibu mkuu wa chama cha usafirishaji (Hakiboa) Lokeni
Adofu alisema kuwa kweli mgomo upo mkoani Kilimanjaro na kwa mkoa wa Arusha walishindwa kwenda
kutokana na fujo ambazo zilikuwa zinafanywa huko ila alibainisha kuwa
mazungumzo yanaendelea na madereva wote wanatakiwa kuingia kazini hadi pale
mazungumzo yatakamilika
“mimi nasema kweli mwenyekiti wetu wa haki boa ameketi na kamanda wa polisi mkoa wa
Kilimanjaro mazungumzo yanaendelea ili kupata suluhu ,lakini wakati
amazungumzo yanaendealea sisi kama haki
boa tumewaamuru madereva wote mkoani Arusha waingie standi wavae sare dereva na
kondakta wake wabebe abiria wawapeleke
mkoani Kilimanjaro kama kawaida na napenda kuwahakikishia usalama wao utakuwa
vizuri kwani kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro ameshaweka ulinzi wa kutosha na tutaendelea kulipa ushuru shilingi 1000
mpaka muafaka upatikane“alisema Adofu
Alisema kuwa lengo kuu la woa kugoma ni kutokana na
kupandishiwa bei ya ushuru kutoka
shilingi 1000 hadi 2000 kw akila kituo pasipo kuuitwa na kukaa chini na
kuongelea swala hilo wao kama
wamiliki
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia