WANANCHI WA KIJIJI CHA KWAITITO WALIA UKAME MBELE YA DC WA HAI

 mkuu wa wilaya  ya Hai Novatus Makunga akiwa anaandika matatizo ambayo yalikuwa yanasemwa na wananchi
wananchi wakiwa wanamsikiliza  mkuu wa wilaya kwa makini
 Wananchi wakiwa wanamsikiliza mkuu wa wilaya kwa makini


Wananchi wa kijiji cha Kwatito wameeiomba serikali kuwapelekea chakula kutokana na ukame unaowakabili unaotokana na kukosa kwa mvua kwa misimu mitatu mfululizo.

Wananchi hao wametoa kilio hicho kwa mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Novatus Makunga katika mkutano wake wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho hicho.

Aidha wameiomba serikali kudhibiti uingiaji wa makundi ya mifugo katika maeneo hayo kwa lengo la kutafuata mabua ya mahindi yaliyonyauka kutokana na ukosefu wa mvua.

kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya Mhe Makunga ameeleza kuwa tayari tathimini ya mahitaji ya chakula imeshakamilika na imetumwa katika ngazi husika.

Aidha aliwataka wananchi hao kuwa tayari kubadilika na kuingia katika kilimo cha mazao yanayostahimili ukame ambapo wilaya itaingia mkakati huo katika msimu ujao wa kilimo kikiwemo kilimo cha Mtama

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia