MJINI MAGHARIBI YATINGA 16 BORA COPA COCA-COLA
Mjini
Magharibi imetinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Copa Coca-Cola baada
ya leo (Julai 4 mwaka huu) kuilaza Tanga bao 1-0 katika mchezo
uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Bao
la washindi katika mechi hiyo ya kundi B lilifungwa dakika ya 68 na
Juma Ally. Kwa matokeo hayo Mjini Magharibi ambayo imemalizika mechi
zake imefikisha pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine
katika kundi hilo.
Mbeya
imejipatia ushindi wa pili mfululizo katika kundi lake la C baada ya
leo kuifunga Mara bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Tanganyika
Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam. Mshambuliaji John Jerome alifunga
bao hilo pekee dakika ya 43.
Licha
ya ushindi huo Mbeya wameshindwa kukata tiketi ya 16 bora kwani
wamemaliza mechi zao wakiwa na pointi sita tu. Timu za Dodoma yenye
pointi 12 na Kinondoni ambayo imefikisha pointi 10 na mechi moja mkononi
ndizo zilizofuzu kucheza 16 bora kutoka kundi hilo.
Pwani
imepata ushindi wake wa kwanza katika kundi lake la D baada ya leo
kuichapa Kagera mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Nyumbu
mkoani Pwani. Mabao ya washindi yalifungwa na Cotiveno Ngaga dakika ya
19, Abdallah Juma dakika ya 30 na Salum Ame dakika ya 68.
Kagera
ambayo imebakiza mechi moja dhidi ya Shinyanga ikiwa na pointi sita
ilipata bao dakika ya 42 kupitia kwa Athuman Kassim. Nazo Ruvuma na
Arusha zimetoka suluhu katika mechi ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa
Tamco.
WACHEZAJI 11 WAMALIZA MIKATABA COASTAL UNION
Wachezaji
11 wamemaliza mikataba yao ya kuichezea timu ya Coastal Union ya Tanga
inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na sasa wako huru kujiunga na
klabu yoyote.
Kwa
mujibu wa Coastal Union, wachezaji hao ni Ben Mwalala, Samwel Temu,
Francis Busungu, Ahmed Shiboli, Lawrence Mugia, Daudi Chengula, Godfrey
Mmasa, Mwinyi Abdulrahman, Sabri Ramadhan China, Soud Abdallah na
Ramadhan Wasso.
Uhamisho
wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika
Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa
Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.
Kwa
klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni
kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia
Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia