WANANCHI WA BABATI VIJIJINI WALALAMIKIA SEREKALI

Mwananchi akichangia jambo

 Mwenyekiti wa kijiji cha Magugu Omary Mazinde akiwa kwenye mkutano mkuu wa kawaida wa kijiji hicho nyuma yake mwenye gauni la zambarau ni diwani wa kata ya Magugu Rehema Oamari  wakifuatilia mkutano huo wilayani Babati vijijini

Wakazi wa kijiji cha mdori wilayani Babati vijijini wameilalamikia serekali wilayani humo kwa kuwanyima fursa ya kupata kitoweo cha samaki kwa kutoa amri ya kuyafunga maziwa ya Burunge na Manyara kwa madai huko ni kukiuka sheria walizojiwekea.

Malalamiko hayo wameyatoa wakati LIBENEKE LA KASKAZINI lilipotembelea kijijni hapo kutaka kujua wameipokeaje Amri ya mh.Dc Khalidi Mandia aliyoitoa ya kuendelea kuyafunga maziwa hayo wakati sheria ya uvuvi wilayani humo inawataka kwa sasa kuendelea na uvuvi kwani maziwa hayo hufungwa kuanzi dec30 hadi july1.

Walisema kuwa huko ni kushindwa kwa idara ya uvuvi kulishughulikia suala la uvuvi haramu kwenye kipindi cha kuachia samaki kuzaana na kuwa wao wanaingia kwenye mtego wa panya bila sababu yeyote.

Moja wa wakazi wa kijiji hicho Matei Laizer alisema kuwa anachojua yeye kuwa uongozi wa kijiji na halmashauri imeshindwa kuweka ushirikiano kwa wananchi kwenye ulinzi shirikishi na kuwa wao wamekuwa mbuzi wa kafara kwa wavuvi haramu ambao wanavua mchana kweupe bila ya uongozi wa kijiji kuwachukulia hatua unadhani viongozi wa kijiji hawawajui wanaovua wapo na wengine wanaishi majumbani mwao na wanawapoke bila ya kificho.

Laizer akawataka sheria ifuate mkondo wake kwa viongozi na wananchi watakaobainika kuchukuliwa hatua kali niabu kwa serekali kutoa amri ya kuzivunja sheria kwa kuwachia wachache kufaidi rasilimali zetu kwa manufaa ya wachache na kumtaka Dc kutokukurupuka kutoa amri kama hizo na badala yake kuangalia tatizo lipo wapi kuwaumiza wanaolitegemea ziwa hili kuendesha maisha yao.

Mmoja wa wavuvi katika ziwa hilo Huseini Juma alisema kuwa kwasasa familia yake inazidi kupata tabu kwa miezi mingine kwa uzembe wa wachache kutotii sheria na serekali kushindwa kuwafuatilia huku ni kuumiza wengi kwa faida ya wachache.

Sakata hilo limetokana na kauli yam h.dc aliyoitoa kwenye kikao cha baraza la madiwani wa mji wa babati mwishoni mwa mwezi uliopita akisema kuwa imetokana na kikao cha wakuu wa mikoa katika kikao cha ujirani mwema kuangalia athari za mazalia ya samaki na utumiaji wa kokoro katika uvuvi hali iliyopoelekea samaki katika maziwa hayo kupungua kwa kasi na kuhatarisha uwepo wao.

Uvuvi haramu umekuwa ni changamoto kubwa kwa idara za uvuvi kwenye mikoa ya Kilimanjaro,na manyara kwani idara za uvuvi zimekuwa na changamoto mbali mbali ikiwemo vitendea kazi vya kisasa ikiwemo boti Mafuta,na fedha za kujikimu kwani uvuvi umekuwa ukifanyika kwa kuvizia badala ya doria endelevu na baadhi ya halmashauri kuwatupia lawama wananchi kushindwa kutoa taarifa kwa wakati

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia