KAMPUNI YA UWINDAJI YATUHUMIWA KUMPIGA RISASI MWINDAJI
KAMPUNI ya uwindaji ya
Mwiba holdings ya jijini Arusha inayomilikiwa na wakili maarufu nchini,Nyaga
Mawala imeingia kwenye kashfa nzito ,baada ya askari wake kummiminia risasi na
kumjeruhi vibaya mfugaji ambaye amelazwa
kwenye chumba cha wagonjwa mahututi(ICU)wilayani Arumeru.
Mfugaji huyo ametambulika
kwa Kitabungéta Kitajuri(25)mkazi wa kijiji cha Kakesyu ,Endulen wilaya ya
Ngorongoro amenusurika kufa baada ya askari wa kampuni ya uwindaji ya Mwiba ya jijini Arusha ,kumjeruhi kwa
risasi wakati akitafuta mifugo yake iliyokuwa imepotea.
Akizungumza kwa tabu katika
chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)katika hospitali ya Selian
alipolazwa,Kitajuri alisema kuwa tukio hilo lilitokea julai 8 mwaka huu majira
ya saa 8 mchana baada ya askari hao kumkuta kandokando ya eneo la uwindaji .
Kwa mujibu wa Kitajuri ,askari hao wa wanyama pori walikuwa watatu kwenye
gari la wazi aina ya Landrover ,na kwamba baada ya kumwona walisimamisha gari na
mmoja wa askari hao alimfyatuli risasi za kutosha na kumjeruhi vibaya sanjali
na kumvunja mkono wa kushoto.
‘’hao askari walikuwa
watatu kwenye gari walioniona walisimamisha gari bila hata ya kuniuliza
walianza kunifyatulia risasi na baada ya kuona nimeanguka chini waliwasha gari
na kuondoka kwa mwendo mkali’’alisema Kitajuli
Alifafanua kuwa siku ya tukio majira ya mchana alipoteza
ngómbe wake 10 na kuhisi kwamba pengine watakuwa wamekimbilia kwenye chemchem
ya maji iliyopo kando kando na eneo la uwindaji la wakili Mawala,ambapo
alipokaribia ndipo alipokutana na askari hao.
Akizungumzia tukio hilo
shemeji yake aliyejitambulisha kwa jina la Shegwega Kidamani ambaye anamuunguza
alisema kuwa walipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kuwa ndugu yake huyo
alikuwa amepatwa mkasa wa kupigwa risasi
na askari wa wanyama pori na kwamba alikuwa na hai mbaya.
Alisema walijaribu
kufuatilia na kumkuta amelala kwenye majani bila msaada wowote damu nyingi
zikivuja,ndipo waipoamua kumpeleka hospitali ya Enduleni iliyopo wilayani humo.
Aliongeza kuwa ilipofika siku ya jumanne tarehe 10
walimhamishia katika hospitali ya Seliani ,Ngaramtoni iliyopo wilayani Arumeru kwa
lengo la kuondoa risasi zilizokuwa zimekwama
mwilini mwake.
Kwa mujibu wa daktari
waliokuwa wakimtibu hopitalini hapo ambaye aligoma kutaja jina lake akidai si
msemeji ,alisema kuwa hali ya mfugaji huyo bado ni mbaya na kwamba bado yupo
kwenye uangalizi wa hali ya juu na jitihada za kuondoa risasi zilizokuwa mwili
mwae walikuwa bado wanaendelea.
Kampuni ya Mwiba Holding
ipo mpakani mwa mkoa wa shinyanga katika
wilaya ya Maswa na kwamba mara nyingi kampuni hiyo imekuwa ikikumbwa na matukio
ya kupiga risasi wananchi wanaoishi eneo hilo na maiti zao zimekuwa zikiokotwa
bila kujua ameuawa lini.
Jitihada za kumpata mmiliki
wa kampuni hiyo Nyaga Mawala zilishindikana baada ya kutopokea simu licha ya
kutafutwa mara kadhaa kupitia simu yake ya mkononi ,ambapo simu ilikuwa ikiita
bila kupokelewa hata alipotumiwa ujumbe wa simu hakuweza kutoa ushirikiano.
Kwa upande wa kamanda wa
polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alipoulizwa alisema kuwa alikuwa bado
hajapata taarifa na kuahidai kuzifuatilia.
‘’inawezekana tatizo kama
hilo lipo ila wahusika pengine hawauripoti polisi ila nitafuatilia’’alisema
Sabasi
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia