EUGENE AWA BALOZI WA NAURA SPRING HOTEL HUKU MAGEDALENA AKITWAA TAJI LA TOP MODEL

Magedalena akipita jukwaani na vazi la kimasai
Mrembo wa Ilala, Magdalena Roy, usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kunyakua taji la mrembo wa pili kuingia hatua ya nusu fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012 baada ya kuwashinda warembo wengine 29 na kutwaa taji la Top Model.

Magdalena aliibuka mshindi katika shindano dogo la Redd's Miss Tanzania lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kimataifa ya Naura Springs jijini Arusha.

Kwa matokeo hayo Top Model, Magadalena Roy anaungana na Miss Photogenic, Lucy Stephano katika nusu fainali hiyo na kukaa tayari kusubiri warembo wengine 13 watakaoungana katika Nusu fainali hizo.

Taji la TOP MODEL lilikuwa linashikiliwa na mrembo wa Temeke, Mwajabu Juma.
Mrembo kutoka Mkoa wa Mara na Miss Kanda ya Ziwa 2012, Eugene Fabian nae alifanikiwa kutwaa taji la Ubalozi wa Hotel ya Naura Spring ya jijini Arusha. 

Egene alitangazwa kunyakua taji hilo usiku wa kuamkia leo wakati wa shindano dogo la Redds Miss Tanzania 2012 la kumsaka Top Model ambaye pia ataingia katika hatua ya 15 bora ya Shindano hilo la taifa la Miss Tanzania. Awali taji la Balozi wa Naura Spring Hotel lilikuwa likishikiliwa na Neema Joel.

walio ingia tano bora hawa hapa

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia