KONGAMANO LA KWANZA UTALII NCHI ZA AFRIKA KUFANYIKA ARUSHA
| naibu waziri wa utalii Lazaro Nyalandu akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano la utalii linalianza kesho katika jumba la mikutano la AICC jijini hapa |
Waandishi wa habari wa mkoa wa arusha wakiwa wanfanya kazi yao katika mkutano wao na naibu waziri
Makamu wa
rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa
Kufungua Kongamano la Kwanza Afrika kuhusu usimamizi wa Utalii Endelevu katika
Hifadhi za Taifa.
Akizungumza
na vyombo vya habari Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Lazaro
Nyalandu alisema kuwa Kongamano hilo linatarajiwa kuanza rasmi October 15-18
katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa (AICC) uliopo jijini Arusha.
Bw. Nyalandu
alisema kuwa kongamano hilo lina lengo la Kubadilishana uzoefu kuhusu fursa,
changamoto, zilizopo katika uhifadhi katika kukuza uchumi.
Alisema kuwa
Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kama mapori ya akiba,hifadhi za taifa
ngorongoro na hifadhi za asili za misitu, pia vivutio vya asili na kiutamaduni
kama michoro ya mapangoni iliyopo Kondoa Irangi,eneo la kihistori la olduvai na
nyayo za kale za laytoli zilizopo
ngorongoro.
Aidha alisema
kuwa sekta ya utalii inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitanda ambapo
alisema kuwa kwa ujumla swala hilo ni changamoto kubwa ambapo serikali
imejipanga kukabiliana nalo ili kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inakuwa na
kuongeza pato la taifa.
“Serikali
inafanya kila ambalo linawezekana ili kuweza ili tuweze kuhakikisha kuwa
vitanda vinatosha pamoja na miundo mbinu kuwa bora zaidi ili viweze kutosha
wageni ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwa urais zaidi.”alisema bw.Nyaladu
Pia alifafanua
kuwa jumla ya washiriki 412 wanategemewa kushiriki kutokanchi 40 za bara la afrika wakiwemo mawaziri kumi na tatu
ambapo amesema kuwa washiriki 242 ambapo ni sawa na asilimia 59% watakuwa ni
watanzania na asilimia 41% ni wageni
kutoka nchi mbalimbali za bara la afrika.
Alisema kuwa
Kongamano hilo limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa lenye makao makuu
yake nchini Hispania kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia