MAONYESHO YA SOBER HOUSES RECOVERY ART EXHIBITION, ALLIANCE FRANCAISE, DAR ES SALAAM, TAREHE 17 – 19, OCTOBA, 2012.
Drug Free Zanzibar (DFA) imeandaa maenyesho ya Sober House Recovery Art
Exhibition. Katika maonyesho hayo vijana wanaoishi katika nyumba za
kurekibishia tabia waathirika wa dawa za kulevya (Sober Houses) watapata
fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika fani za uchoraji, ushonaji na
uchongaji wa vitu mbalimbali. Pia wanajishughulisha mafunzo ya lugha za
kiingereza na kifaransa, yoga, drama pamoja na shughuli mbalimbali za
uzalishaji mali .“Sober Houses” hizi zimesaidia mamia kwa mamia ya
vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini kuachana na matumizi ya dawa za
kulevya wakiwemo watu maarufu katika fani mbalimbali. Lengo la haya yote
ni kuwasaidia vijana ili warudi katika mstari na kurudi katika jamii
zao stahiki
Maonyesho haya yatafanyika katika ukumbi wa Alliance Francaise Upanga
kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 19/10/2012, saa tatu asubuhi mpaka saa
kumi na mbili jioni. Kiiingilio ni bure na wote mnakaribishwa kushiriki
ili kuwasaidia na kuwatia moyo vijana wetu ambao wameamua kuachana na
matumizi ya dawa za kulevya na kuwa mfano bora kwa vijana wenzao ambao
bado wanajishughulisha na matumizi pamoja na biashara ya dawa hizi
Kwa maelezo zaidi, kusaidia pamoja na ushauri unaweza kuwasiliana na
ndg. Suleiman Mauly 0782 000426 au ndg. Alois Ngonyani 0713 334423/0686
334423
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia