RWANDA YAKANA KUKOSA FEDHA KUGHARIMIA KESI YA UWINKINDI
Rwanda, Jumanne imekanusha ripoti kwamba timu ya utetezi ya mshitakiwa wa
mauaji ya kimbari, Mchungaji Jean Uwinkindi imekosa fedha za kuwawezesha kufanya
upelelezi na kuwatafuta mashahidi wa kumtetea mteja wao.
Uwinkindi
ni mshitakiwa wa kwanza wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
(ICTR) kesi yake kuhamishiwa nchini Rwanda,kusikilizwa katika mahakama ya nchi
hiyo.
Gatera
Gashabana,Wakili wa utetezi wa Uwinkindi alitoa malalamiko ya kukosekana kwa
fedha, kwa mujibu wa msimamizi wa mwenendo wa kesi hiyo wa ICTR, Anees Ahmed.
Lakini kwa upande wake, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Rwanda, Martin Ngoga alisema
Jumanne kwamba hakuna uhaba wa fedha kugharimia kesi hiyo.
‘’Serikali
inajua majukumu yake ya kuwezesha upande wa utetezi chini ya mfumo wa msaada wa
kisheria,’’ Ngoga aliliambia Shirika la Habari la Hirondelle kwa simu.
‘’Shughuli yoyote ya upande wa utetezi inayoruhusiwa na mahakama italipwa.Hakuna
uhaba wa fedha kwa ajili hiyo.’’
‘’Kama
upande wa utetezi unataka kufanya shughuli yoyote, hawana budi kuiomba
mahakama,’’ Ngoga aliiambia Hirondelle. Alisema hakuna ombi la aina hiyo mbele
ya jaji na kwamba ‘’hakuna haja ya kupiga kelele kwa jambo ambalo halijafikishwa
mbele ya mamlaka husika.’’
Alipokuwa
chini ya kizuizi cha ICTR, Mchungaji Uwinkindi kama mtu asiyekuwa na uwezo wa
kujilipia huduma za kisheria, alikuwa anapewa huduma hiyo na mahakama hiyo ya
Umoja wa Mataifa.Lakini Mbele ya mahakama ya Rwanda, gharama za msaada wa
kisheria zinatakiwa kulipwa na serikali ya Rwanda.
Kwa mujibu wa ripoti ya msimamizi wa
mwenendo wa kesi hiyo, msaada wa kisheria unaotolewa kwa Wakili Kiongozi na
Msaidizi wake unagharimia huduma tu na hauruhusu kulipia gharama za kukodisha
wapelelezi wa kesi au gharama za kuwatafuta mashahidi watarajiwa, kuchukua
maelezo yao na kuhakikisha kuwepo mbele ya mahakama wanapohitajika.
ICTR
iliamuru kuhamishwa kwa kesi ya Uwinkindi kwenda kusikilizwa nchini Rwanda Juni
mwaka jana na Mahakama ya Rufaa ilithibitisha uamuzi huo Desemba, 2011.
Uwinkindi alihamishiwa nchini Rwanda Aprili 19, 2012.
Wafanyakazi
wawili wa ICTR waliteuliwa kuwa wasimamizi wa muda wa mwenendo wa kesi hadi hapo
makubaliano yatakapokamilishwa ya kupata wasimamizi kutoka Kamisheni ya Afrika
ya Haki za Binadamu na Watu(ACHPR).
Mchungaji
Uwinkindi anashitakiwa kwa mauaji ya kimbari na kuteketeza kizazi. Kwa mujibu wa
Msimamizi wa ICTR, upande wa mwendesha mashitaka uko tayari kuanza kusikilizwa
kwa kesi hiyo.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia