SEREKALI YASISITIZAN KUSHIRIKIANA NA WADAU KATIKA KUENDELEZA KILIMO
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam mara mara ya kuongoza mkutano maalum wa
Mpango wa kukuza kilimo kusini mwa Tanzania (SAGCOT), akizungumzia
umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya kilimo, kulia ni Waziri wan chi
Ofisi ya waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu na Kushoto
ni Waziri wa Kilimo, Bw. Christopher Chiza.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Serikali
ya Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta
binafsi na wadau wengine ili kufikia mapinduzi ya kilimo hapa nchini na
hivyo kupatikana usalama wa chakula na maendeleo.
Msimamo
huo umetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano
mkubwa wa kilimo unaofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkutano
huo wa siku mbili umetayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Kituo cha mpango maalum wa
uendelezaji kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
Mkutano
huo unalenga kuvutia wawekezaji katika maeneo ya kilimo, biashara na
miradi ya maendeleo kijamii na kiuchumi katika eneo la SAGCOT.
“Ushirikiano
uliopo kati ya serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo, wakulima na
wadau wengine wa kilimo umesaidia kuendeleza sekta hii hapa nchini,”
alisema.
Waziri
Mkuu aliyashukuru makampuni 20 ambayo tayari yameshatoa ahadi ya
kuwekeza katika sekta ya kilimo Tanzania katika miaka ijayo na wakati
huo huo akaitaka sekta binafsi kufanya uamuzi zaidi wa kuwekeza zaidi
katika sekta hiyo.
Hata
hivyo alisisitiza kwamba wawekezaji wote katika ukanda wa SAGCOT
watapewa kipaumbele pale ambapo uwekezaji wao unalenga pia kushirikisha
wakulima wadogowadogo..
“Ni
muhimu kusisitiza kwamba tunahitaji zaidi uwekezaji ambao utajali
kushirikiana na wakulima wadogo na wajasiriamali wadogo na wa kati,”
alisema.
Alisisitiza
kwamba hata mapendekezo ya sera za uwekezaji katika kilimo zitoe
kipaumbele kueleza jinsi wakulima wadogo na watanzania wa kawaida
watakavyofaidika na uwekezaji katika ukanda wa SAGCOT.
Waziri
Mkuu aliwahakikishia wawekezaji kwamba kupitia sheria mbalimbali
Tanzania inatoa vivutio vingi na vizuri kulinganisha na nchi nyingine za
Afrika.
“Kuwekeza Tanzania pia kunawahakikishia soko la uhakika katika eneo hili la Afrika,” alisema.
Alisema Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohakikisha usalama wa wawekezaji.
Akitoa
mada katika mkutano huo, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi
Christopher Chiza alitaja baadhi ya maeneo yanayolengwa katika
uwekezaji SAGCOT kama kilimo cha miwa, matunda, ufugaji, nafaka na mazao
ya misitu.
Katika
siku ya pili ya mkutano huo wawekezaji watapata fursa ya kutembelea
maeneo maalum ya miradi pamoja na kuangalia miradi ya kuimarisha
miundombinu katika ukanda huo wa SAGCOT.
SAGCOT ni
mpango unaoshirikisha sekta binafsi na ya umma unaotegemewa kuleta
mapinduzi makubwa katika usalama wa chakula nchini kwa kushirikisha pia
wakulima wadogo wadogo katika mazingira endelevu.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia