MDOGO WA MTANGAZAJI WA ITV OFOO SARO AELEZA JINSI TUKIO LA KUPIGWA RISASI LILIVYOTOKEA
MDOGO WAKE UFOO SARO AELEZEA TUKIO LA KUPIGWA RISASI DADA NA MAMA YAKE LILIVYOTOKEA, YEYE NA WENZAKE WALIJIFICHA JUU YA DALI
Mdogo
wake mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Ufoo Saro aliyejitambulisha
kwa jina la Goodluck ameelezea jinsi ambavyo tukio lilotokea nyumbani
kwao juzi majira ya saa moja na nusu asubuhi ambapo shemeji yake Anthery
Mushi alimpiga risasi dada yake na kumjeruhi tumboni na begani, na
kumuua mama yake (mama mkwe) na kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujipiga
risasi.
“Tulisikia
sauti ya risasi sebuleni…na hapo mama akawa anatuita anasema njooni
hapa nakufa, tulipotoka nje tukakuta na dada nae ndo yuko chini,
akatuambia rudini ndani anataka kutuua wote hawa, ndo tukarudi ndani.
Baada ya kurudi ndani ndo akaanza kupiga risasi milangoni na madirishani
akawa anasema tokeni nje nataka niwauwe.” Alisema Goodluck.
“Na
sisi tukakimbia tukapanda juu dalini baada ya kusikia mlango wetu
umeshapigwa sana risasi na dirishani, tukapanda juu ya dali, baada ya
kupanda juu dalini tukasikia mlio wa risasi mbili zinalia tena sebuleni
na hatukuwezi kutoka kule juu dalini. Baadae akatoka akaenda kufungua
gas akawasha moto wa gas, sasa moshi ukawa unakuja kule juu dalini na
hatuwezi kupumua, tukaja tukakuta jiko la gas lile limewaka liko karibu
na pikipiki.
“Baada
ya polisi kuja na kuzunguka nyumba tukakuta mtu mwenyewe amekaa kwenye
kochi na yeye kajiripua risasi. Tukaulizia dada yuko wapi tukaambiwa
wamemuona dada mmoja hapa amechafuka damu amepelekwa Tumbi na pikipiki,
ndo baada ya kufuatilia ndo tunasikia amepelekwa Muhimbili.”
Ufoo
Saro amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na tayari
amefanyiwa upasuaji. Jana kamishina msaidizi wa upelelezi kanda maalum
ya Dar es Salaam Hemed Msangi,amesema kuwa Ufoo amejeruhiwa eneo la
mkononi, begani na tumboni na hali yake inaendelea vizuri.
Chanzo: Taarifa ya habari 100.5 Times fm

0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia