TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI JUU YA AGIZO LA KAMATI YA BUNGE (PAC) KUHUSU VYAMA KUTOKUKAGULIWA NA CAG TANGU MWAKA 2009-2013.
C/HQ/ADM/KUH/18 17/10/2013
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI JUU
YA AGIZO LA KAMATI YA BUNGE (PAC) KUHUSU VYAMA KUTOKUKAGULIWA NA CAG TANGU
MWAKA 2009-2013.
Kutokana
na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuwa
vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha
taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi cha miaka minne mfululizo,
yaani kuanzia mwaka 2009/2010- 2012/2013.
CHADEMA
tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo juu ya taarifa hizo;
i.
Kuwa taarifa hizo sio sahihi na hazina
ukweli kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine, hii ni kutokana na ukweli
kuwa tulishawasilisha taarifa zetu za fedha kwa msajili wa vyama vya siasa na
zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011, 2011/2012 na hili linathibitishwa
na barua ya msajili wa vyama vya siasa yenye Kumb.Na. CDA.112/123/01a/37,
ya tarehe 04 september 2012. Iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya
siasa (nakala imeambatanishwa).
Aidha,
hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/2010, tuliziwasilisha kwa
Msajili wa vyama vya siasa kwa barua yenye Kumb.Na.
C/HQ/ADM/MSJ/04/71 ya tarehe 27 Octoba, 2011. (Nakala ya barua imeambatanishwa)
ii.
Kuhusu taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa
mwaka huu wa fedha 2012/2013, bado haijawasilishwa kwenye ofisi za msajili wa
vyama kutokana na barua ya msajili wa vyama vya siasa ya Novemba 26, 2012 yenye
Kumb.Na.DA.112/123/16A/97 ambayo
ilikuwa na maelekezo kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa, iliyokuwa
inajibu barua tuliyomwandikia tukitaka kupata ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa
hesabu za chama kutakiwa kufanywa na CAG na alitujibu kuwa “tumefanya mawasiliano na Mkaguzi
na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali (CAG) kwa ufafanuzi wa jambo hili na
tutawafahamisha ipasavyo kuhusu malipo/gharama mliyotakiwa kulipa katika
ukaguzi wa Mahesabu hayo”; mpaka leo hatujawahi kupata ufafanuzi huo
pamoja na ukweli kuwa tumeshafunga hesabu zetu za mwaka kama chama (barua imeambatanishwa).
iii.
Kuhusu taarifa ya fedha kutoka nje ya nchi,
CHADEMA tumekuwa tukiwasilisha taarifa zetu kila mara tunapopata fedha kwa
ajili ya mafunzo na programu nyingine mbalimbali za chama kama ambavyo msajili
alituandikia barua tarehe 19 Agosti 2013 yenye Kumb. Na.DA.112/123/16a/10 iliyokuwa ni taarifa ya mapato
yatokanayo na michango au misaada toka nje ya nchi, alisema “tunashukuru
kwa taarifa hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya vyama vya siasa” (imeambatanishwa
barua husika )
iv.
Kuhusu Taarifa za gharama za uchaguzi kwa
mwaka 2010 , tuliwasilisha taarifa hiyo na Msajili alikiri kuwa ni vyama viwili
tu ndiyo vilikidhi utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi kwa ukaguzi wa
marejesho, hii inathibitishwa na barua ya Msajili yenye Kumb.Na. CDB.173/205/01/23 ya tarehe 16 April, 2012. (Nakala
imeambatanishwa)
Tunapenda
kuwahakikishia watanzania kuwa CHADEMA ndiyo ambayo tulidai CAG awe na mamlaka ya kukagua fedha za
vyama vya siasa ili taarifa zake ziwekwe hadharani na tutaendelea kutoa
ushirikiano kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote, kuhakikisha sheria hii
inatekelezwa ipasavyo kuhakikisha uwazi kwenye mapato na matumizi ya vyama vya
siasa.
Aidha,
kama ambavyo siku zote tumesimamia na kusisitiza, tunamtaka CAG akague fedha
zote za vyama na sio ruzuku tu kama ambavyo kamati ya Bunge inataka iwe.
Imetolewa leo Alhamis, Oktoba 17, 2013;
……………………….
Antony C. Komu
Katibu wa Baraza la Wadhamini.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia