SEREKALI IMETAKIWA KUTHIBITI DAWA FEKI
washiriki wa semina ya siku mbili ya kujadili masuala m,bali mbali ya
kilimo hapa nchini wakiwemo watengenezaji,waagizaji na wasambazaji wa
dawa za mimea hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza
kwa semina hiyo
Serekali na
wadau wa chama wa watengenezaji,waagizaji na wasambazaji wa dawa za mimea na
mbegu hapa nchini(CROP LIFE TANZANIA)wameanza kupambana na uingiuzaji wa dawa
feki za mazao katika kuongeza thamani ya mazao na kipato kwa mkulima hapa
nchini.
Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho hapa nchini Harish Dhutia wakati
alipokuwa akiongea na wanahabari kwenye semina ya siku mbili kwa wadau hao
pamoja na mwakilishi wa wizara ya kilimo na chakula na mkurugenzi wa TPRI.
Dhutia
alisema kuwa kumekuwapo na ongezeko la madawa feki kwenye soko la bidhaa hizo
hapa nchini kiasi kuwa kumekuwa kukiwanyima wakulima ongezeko la thamani ya
mazao na kipato hivyo wameamua kuanzisha mapambano hayo kudhibiti uingizaji wa
dawa feki.
“Unajua
udhibiti wa dawa feki za kilimo unahitaji ushirikiano kati ya wadau na serekali
na hasa matumizi sahihi ya dawa za kilimo katika kukuza mimea na
tusiposhirikiana tutashindwa kufikia malengo ya serekali ya matokeo makubwa
sasa katika sekta ya kilimo”alisema Dhutia.
Aidha
mwenyekiti huyo alitanabaisha sasa kumekuwepo na matumizi ya vifungashia vya
dawa na wakulima wamekuwa wakivitupa ovyo kiasi cha kuharibu mazingira na
kuongeza sumu mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwa hatari kwa afya za binadamu
na mimea hvyo kampeni hii itakwenda sambamba na kutoa elimu kwa wakulima hapa
nchini.
Kwa upande
wake mkurugenzi wa TPRI alisema kuwa serekali na sheria za kudhibiti ongezeko
la dawa feki imekuwa ni tatizo kwao kwani bajeti yao imekuwa finyu katika
kudhibiti suala hilo na kuomba serekali kuongeza bajeti ili nao waweze kuingia
kwa undani kwenye kudhibiti dawa feki hapa nchini.
Aktanabaisha
kuwa serekali ipo makini kwenye suala hilo na kuwa mipango ya kuongeza ongezeko
la chakula ipo kweny mpango wa matokeo makubwa sasa unaoendeshwa na srekali hii
ni moja ya vipaumbele vya serekali.
Hapa umeona
tunaanza na udhibiti wa vifungashia vya madawa hususani makopo ya dawa kwani
yamekuwa yakiharibu mazingira na ni sumu kwa binadamu kama hayatawekwa katika
mpangilio na kuyaharibu itakuwa tunafanya kazi bure kwenye sekta ya kilimo
ambayo ni muhimili wa uchumi wa taifa hili
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia