ASASI mbalimbali zinazojihusisha na mapambano ya udhibiti wa ugonjwa wa ukimwi,
zimetakiwa kuangalia upya mipangoyao ili kuongeza nguvu zaidi ili kutokomeza
maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo,kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba mosi iliyoaadhimishwa kimkoa
wilayani Longido.
Aidha amezionya asasi na mashirika yanayotumia migongo yawagonjwa kujinufaisha na
misaada inayotolewa na wahisani kuacha mara moja tabia hiyo.
’’Kuna
baadhi yaasasi zimeandikishwa kufanya kazi
zipo zinazotumia misaada na fedha za
walengwa kujinufaisha huku walengwa wakibakia bila misaada’’alisema mulongo.
Akaziagizahalmashauri za wilaya kufuatilia nakusimamia mipango ya mashirika hayo na kuzitaka taasisi hizo kuhakikishazinatoa taarifa zake serikali ,wakurugenzi afuatilie na kutambua misaada yote inayotolewa
zikiwemofedha kuoana ka,a zinawafikia walengwa.
“walioanzishavituo vya Yatima wafuatiliwe ambaowatabainika kutumia misaada hiyo ya yatima washughulikiwe mara moja kwa kuwawanatumia migongo ya yatima kujinufaisha na hilo halikubaliki kabisa na wala
halina nafasi’aslisema, mulongo
.
Akaziagizahalmashauri kuwatambua waathirika ili waweze kujiunga kwenye vikundi halafu
wapatiwe mikopo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi,kutokana na serikali imetengamilioni 600 kwa ajili ya kuwawezesha wagonjwa na waathirika wa ukimwi kuanzishashughuli za kiuchumi,
Piaakazitaka halmashauri na asasi hizo kukaa pamoja na kuchambus vipaumbele katika
mapambano ya ukimei kuzingatia mahitaji ya halmasauri husika’Sitaki kusikia
kuna vifo tena vinavyotokana na ukosefu wa wa dawa , unyanyapaa na unyasnyasaji
wowote ule ,lengolaserikali nikupunguza vifo na maambukizi nasi vinginevyo.
Mkuu wamkoa amesema kuwa hafurahishwi na kazi iliyokwisha fanywa na mashirika hayo
kutokana na kuwepo ongezeko la ukimwi wakati yakidai yanatoa elimu kwa umma
namna ya kupunguza maambukizi hayo
.Amesema mkoa wa Arusha una mashirika yasiyo ya kiserikali 452 ,asasi 15 licha ya
kushirikiana na serikali katika mapambano hayo bado juhudi zaidi zinahitajika.
Amevikemea vyombo vya afya ambavyo vimekuwa vikivujisha siri za wagonjwa kwa watu
wasiohusika akawaagiza waratibu wa ukimwi wa ngazi zote kuanzia mkoa hadi mtaa
kufuatilia ili maadili ya kitabibu yanavyotaka taarifa za wagonjwa ziwe ni siri
yadumishwe.
Amesema mkoa wa Arusha una jumla ya watu 36,000katiyao ni wanawake 25,000 ambao
wamejisajili katika hosipitali, Zahanatina vituo vyaafya kwa ajili ya kuanza dawa za kupunguza makali ya ukimwi hivyolazima tujitazame upya takwimu hizo zinatisha.
Amewatakawanawake kuwanapotongozwa waseme haadanganyikileng nikukwepa kupata
maambukizipia waliokwisha athirika wasijifiche majumbani bali wajitokeze na kujisajili ili waweze kupatiwa misaada mbalmbali.
Amesema yeyote atakaetambuliwa hatapotezamaisha yake labda kwa uweo wa mungu tu hivyo wajitokeze wapime afya zao.
Awali akisoma taarifa afisa maendeleo ya jamii mkoa waArusha, Blandina Nkini, amesema
kuwa jijila Arusha linaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi.
Amesema jiji la Arusha lina 5.0%likifuatiwa na wilaya ya Karatu yenye kiwango cha
3.0% Longido asilimia 2.9% Monduli ni 2.7% Arusha DC, ni 2.00% na Ngorongoro
kiwango cha maambukizi ni 1.3% .
Amesema sababu kuwa ya kuongezeka kwa maambukizi hayo ni kutokana na muingiliano mkubwa
wa watu wakiwemo wageni kutokana na wilaya hizo kuwa ni njia kuu ya biashara ya
utalii na madini.Amesema mkakati uliopo katika mkoa ni kuandaa kamati mpya ya kupambana na ukimwisanjari na kuendelea na upimaji wa hiari wa afya za wananchi
katika maeneo mbalimbali.
Akawataka waliokwisha ambukizwa wasikate tama ya mnaisha na kusema kuwa mkoa
unachangamoto ya kutafuta chanzo cha ongezeko hilo ambalo lilikuwa limeshashuka
na ghafla limeongezzeka
Nkini,
ameomngeza kuwa mkoa wa Arusha kuna watoto 6683waishio kwenye mazingira
magumu na hatarishi na tayari
wameshatambuliwa na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia kwenye mashirika na lengo ni kuwaokoa wasipate maambukizi ya
ukimwi.
Amesema jumla ya vituo 45 vimeendelea kupokea wateja na tayari watu 14151 vituonina kati yao12459 wanatumia dawa za kupunguza makali ya ukimwina magonjwa
nyemelezi.
habari na Mahmoud Ahmad wa libeneke la kaskazini blog