TIMU
YA WABUNGE ya mpira wa miguu imeahidi kurudi na kombe katika michuano
ya kombe la mabunge la Jumuiya ya Afrika mashariki yanayotarajiwa
kuanza kutimua vumbi Disemba 8 huko kampala nchini Uganda.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Arusha ambapo timu hizo za mpira wa miguu na
mpira wa pete zimeweka kambi mwenyekiti wa timu Idd Azan alisema kuwa
maandalizi yanakwenda vizuri na wabu nge karibu wote ambao wanaunda timu
hizo wameshafika kambini tayari.
Kikosi hicho
kilichopo chini ya kocha Kassimu Mjaliwa ambaye ni naibu waziri wa
tamisemi kinaundwa na wachezaji kumi na tano ambao ni wabunge na
wachezaji sita ambao ni watumishi wa bunge.
Azan alisema kuwa
kilichopelekea kwa timu hiyo kushindwa kuchukua ubingwa ni timu ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweka idadi kubwa ya Watumishi huku
ikichezesha wabunge sita tu ambapo kwa mwaka huu utaratibu huo
umefutwa.
“Mwaka jana
tulishindwa kuchukua ubingwa kutokana na timu uliyocheza nayo ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki kuchezesha watumishi wengi na idadi ya wabunge ni
sita tu lakini kama wangechezesha wabunge tu ushindi ulikuwa uwe wa
kwetu”alisema Azan
Kwa upande wake
katibu wa timu hiyo Waziri Kizingiti alisema kuwa wamefurahia maandalizi
na na jumla ya wanamichezo 45 lakini baada ya mazoezi wachezaji 35
wanaounda timu zote mbili wataondoka kuelekea nchini Uganda.
Kizingiti alisema
kuwa changamoto kubwa ni muda mdogo wa mazoezi kutokana na ratiba za
Wabunge lakini kutokana na mazoezi mazuri na mafundisho ya Kocha wana
imanoi kuwa Kombe hilo litarudi nyumbani Tanzania.
Aidha aliongeza
kuwa katika mechi ya Ufunguzi ambayo itachezwa tarehe 9 bunge la
Tanzania itacheza na timu ya Wabunge kutoka Nchini Kenya.
Naye kaptein wa
timu ya wanawake Grace Kiwelu alisema kuwa mazoezi yanaendelea vizuri na
kila kitu kinakwenda sawa na kwamba kombe hilo bado litarudi nyumbani
Tanzania.
Timu ya Bunge ya
wanawake ya mpira wa Pete ilichukua ubingwa katika mashindano
yaliyopita na timu ya Wanaume ya mpira wa miguu ilichukua nafasi ya pili