Abiria Kigamboni taharuki kubwa

Abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni wamekumbwa na taharuki baada ya kivuko hicho kilichokuwa kikielekea Kigamboni kupata hitilafu na kupoteza mwelekeo.

Shuhuda wa tukio hilo, Mwajuma Said alisema nyakati za alasiri kivuko hicho kikiwa kimepakia abiria na mali zao, kilivusha watu lakini kilipofika eneo la Kigamboni tayari kutia nanga kilipata hitilafu na kupoteza mwelekeo.
Said alisema wakati huo kivuko hicho kilikuwa kikitoa moshi mwingi na kwamba, kuna baadhi ya watu walipiga simu Kikosi cha Zimamoto ambacho kilipeleka gari na waokoaji.
Naye John Samuel alilalamika tukio hilo kwamba limetokea kwa sababu kivuko hicho kinafanyishwa kazi usiku na mchana, bila matengenezo na kimekuwa kikitoa moshi mwingi kwa siku tatu mfululizo. “Kwa kweli hali ilikuwa ngumu, tulipata hofu sana maana tulikwama kwenye maji kwa zaidi ya saa mbili, kivuko kilikuwa kikipoteza mwelekeo lakini askari waokoaji walikuwa wapo tayari,” alisema Samuel. Jitihada za kumtafuta msemaji ziligonga mwamba baada ya kukataa kuzungumzia suala hilo.
wa ofisi zinazosimamia vivuko hilo lakini ilielezwa kuwa wahusika wakuu walikuwa ndani ya kivuko hicho wakifanya matengenezo na kwamba kwa sasa hawawezi kuzungumza chochote, watatoa taarifa baadaye.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post