Kituo cha kulelea na kufundishia watoto
cha Children Support Tanzania kilichopo Block T Jijini Mbeya kimeungana na
Ulimwengu mzima katika kuadhimisha siku ya Ulemavu Duniani inayoadhimishwa kila
tarehe 3 Disemba kwa kuzindua uwanja wa mazoezi na mahafali ya Chekechea.
Aidha kituo hicho kimetumia siku hiyo kwa
kusheherekea mahafali ya watoto 15 ambao wanavuka hatua kutoka Chekechea tayari
kwa kujiunga na Darasa la Kwanza mwakani baada ya kupata sifa za kujua kusoma
na kuandika.
Katika Sherehe hizo zilizofanyika katika
Viwanja vya kituo hicho zilizohudhuriwa na wazazi wa wanafunzi wanaosoma hapo
pia umezinduliwa uwanja wa mazoezi unaofahamika kwa jina la CST Fun Village
ambao utakuwa na michezo mbali mbali ya watoto.
Akizungumza katika Sherehe hizo Mwalimu
Mkuu wa Kituo hicho, Omoding James amesema kituo kilianza kupikea watoto tangu
mwaka 2009 baada ya kusajiliwa kikiwa na watoto 13 lakini hadi sasa kuna watoto
zaidi ya 200.
Amesema kituo hicho kinapokea watoto
wenye ulemavu wa akili, Viungo,viziwi, wanaoishi katika mazingira magumu na
watoto wa kawaida ambapo wanafundishwa elimu maalumu ya darasani, ufundi, mziki
na michezo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo hicho Noela Msuya amesema katika maadhimisho ya Ulemavu duniani watanzania
wanapaswa kutowatenga watoto wenye ulemavu kwa kuwa hakuna eneo wala kijiji
kilichotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu bali tunatakiwa kuishi nao
pamoja.
Amesema kauli mbiu ya Siku ya walemavu
Duniani inasema, “Vunja vizuizi, fungua milango kwa jamii jumuishi kwa
maendeleo kwa wote”ambayo inapaswa kuenziwa kwa kuwajengea mazingira ya
kuwapenda walemavu na kuwashirikisha katika shughuli za kiuchumi.
Na TIMU ya libeneke ilipokuwa mbeya
|