MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA MONDULI NA WANACHAMA WAPINGA NA KUTISHIA KUJIUZULU

MZIMU wa kumvua nafasi za uongozialiyekua Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe umeendelea kukitafuna chamahicho baada ya juzi mwenyekiti wake wilaya ya Monduli na mjumbe wa baraza taifa
Amani Silanga na wanachama zaidi ya 1,000 kupinga uamuzi huo na kutishia
kukihama chama hicho.

Akiongea kwa niaba ya kundi lawanachama hao zaidi ya 1,000 aliokua ameambatana nao Silanga alisema uamuzi huowa kamati kuu unahitaji kupitiwa upya kabla ya utekelezaji wake vinginevyo watakihama chama hicho.

Silanga alisema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ambayo wanayo
bado wanaona kuna kasoro kadhaa za kikatiba katika kufikia uamuzi
uliofikiwa na kamati kuuhivyo kuhitaji kupitiwa upya maamyuzi hayo.

''Kwa kuwa kamati kuu imeishatamka maamuzi yake ambayo yanaonekana
kukiuka baadhi ya vipengele vya katiba ya chama hicho tunaomba sasa
suala hilo lipelekwe katika kikao cha baraza kuu la chama hicho ambalo
ndio chombo cha juu ili kujadiliwa na kutolewa uamuzi''alisema
Silanga.

Alisema anaamini katika kila mahali ambapo imejengwa demokrasia ya
kweli na uwazi huamua kulishughulikia suala lolote lile zito kwa
kufuata taratibu na katika ya mahala husika kupitia vyombo vyote vya
juu vya maamuzi ili kudhihirisha uhalali wa maamuzi mazito
inayochukua.

Alisema kwa hoja ya kiongozi kujenga mtandao ndani ya chamaili apate
madaraka ndani ya chama chake si kosa kubwa kama inavyotaka
kuaminishwa kwa wananchi na wala si uasi ama uhaini.

''Mwanasiasa yoyote makini ambae ana malengo makubwa kisiasa ni lazima
atengeneze mtandao wa mumuwezesha kufikia malengo yake ya kisiasa ili
mradi malengo hayosi kukiua chama chake''alisema Silanga.

Alisisitiza kuwa hojahiyo sihoja ya kumuita mtu mhaini kwani hata
katika nchi kama Marekani tumeshuhudia Obama na wenmzake wakitengeneza
mitandao ya kuwawezersha kupata ridhaa ya kuteuliwa na vyama vyao
kugombea kiti cha urais katika nchi hiyo.

Aidha alisema kuwa hata hapa nchini tulishuhudia ama tunashuhudia
mitandao mingi ya wanasiasa kuwawezesha kufikia malengo waliyojiwekea
katika siasa na hawajawahi kuitwa wahaini.

Alitoa wito kwa kamati kuu ya chama hicho na vyombo vingine ndani ya
chama kulinda na kuheshimu mawazo na maoni ya kila mwanachama na
kukemea vitendo ambavyo vimeanzandani ya chama kwa baadhi ya viongozi
kuunda vikosi vyao vya kuteka na kutishia wanachama ambao hawaungi
mkono mtazamo wao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post