BREAKING NEWS

Friday, December 13, 2013

HIVI NDIVYO JINISI JINA LA KIKWETE LILIVYOONGOZA MAZISHI YA MANDELA



Johannesburg. Serikali ya Afrika Kusini, imetoa orodha ya majina ya wakuu wa nchi na Serikali 91 ambao wamethibitisha kushiriki katika shughuli zinazohusiana na safari ya mwisho ya Rais wa kwanza mzalendo wa taifa hilo, Nelson Mandela.
Jina la Rais Jakaya Kikwete ni la kwanza katika orodha hiyo inayowaweka viongozi hao katika makundi kutokana na mabara wanakotoka. Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili jana usiku tayari kuhudhuria Ibada ya Kitaifa ya Mandela ambayo imepangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa FNB (Soccer City).
Kabla ya Serikali kutoa orodha hiyo, Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane alisema wakuu wa nchi na Serikali 53 walikuwa wamethibitisha lakini jana mchana idadi hiyo ilikuwa imeongezeka na kufikia 91. Kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka na kuzidi 100.
Msemaji wa Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini, Clayson Monyela aliwataja marais wengine kutoka Afrika kuwa ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Joseph Kabila, Hifikepunye Pohamba wa Namibia, Mike Sall wa Senegal, Allessane Ouattara wa Cote d’Ivoire, Goodluck Jonathan wa Nigeria, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Dennis Sassou-Nguesso wa Congo Brazaville, John Dramani wa Ghana na Ali Bongo wa Gabon.
Kutoka Amerika ya Kusini ni marais Nicolus Maduro Moros wa Venezuela na Dilma Rousseff wa Brazil ambaye ataambatana na marais wanne wastaafu wa nchini kwake.
Waziri Mkuu wa Bahamas, Perry Christie, Rais wa Guyana, Donad Ramotar, Rais wa Haiti, Michael Martelly na Rais wa Jamaica, Portia Miller, wakati kutoka Asia, kutakuwa na marais Pranab Mukherjee wa India na Hamid Karzai wa Afghanistan.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbot, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
Tayari Rais wa Marekani, Barrack Obama na mkewe Michelle walishathibitisha kushiriki, pia watangulizi wake, Bill Clinton, George W. Bush na Jimmy Carter wanatarajiwa kushiriki katika mazishi ya Mandela yatakayofanyika Qunu, Mthatha Jumapili.
Armando Guebuza wa Msumbiji, , Abdelkader Bensalah wa Algeria, Makamu wa Rais wa Angola, Manuel Vicente, Rais wa Niger, Issoufou Mahamdou, Kaimu Rais wa Agentina, Amado Boudou, Waziri Mkuu wa New Zealand, John Key na Rais wa Bangladesh, Abdul Hamid MD Abdul.
Malkia Haakon wa Norway, Mfalme wa Philippe wa Ubelgiji, Rais wa Pakistan, Mamnoon Hussain, Rais wa Benin, Boni Yayi, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Rais wa Botswana, Seretse Ian Khama, Rais wa Ureno, Anibal Cavaco Silva na Mfalme wa Saudi Arabia, Muqrin bin Abdulaziz Al-Saud, Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, Rais wa Saharawi, Mohamed Abdelaziz, Waziri Mkuu wa Canada,
Stephen Harper wa Chad, Idriss Deby Itno, Rais wa Serbia, Tomisla

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates