JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu ya mdomo: 255 22 2460
735/2460 706-8
FAKSI: 255 22 2460 735/700 S.L.P.
3056
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Ref. No.: TMA/1622 20 Juni, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
MWELEKEO WA HALI
YA JOTO NA MVUA KATIKA KIPINDI CHA JUNI
HADI AGOSTI 2014
Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa, joto na mvua katika
kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA) 2014.
1.
MIFUMO YA HALI YA HEWA
Mifumo ya hali ya hewa inaonesha uwezekano wa
kuongezeka kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya
Pasfiki kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2014. Ongezeko kidogo la joto
linatarajiwa katika ukanda wa magharibi ya bahari ya Hindi. Aidha joto katika
bahari ya Atlantik linatarajiwa kuwa chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa
kusababisha upepo kuvuma kutoka magharibi ukielekea mashariki katika maeneo
mengi ya nchi. Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la
ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi katika
kipindi cha miezi ya Juni hadi
Agosti2014. Hali hii inatarajiwa
kusababisha hali ya baridi katika kipindi hicho. Aidha, vipindi vifupi vya mvua
za vinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa Ziwa Viktoria, ukanda wa
pwani na katika maeneo ya miinuko.
2: VIWANGO VYA
CHINI VYA JOTO NA MVUA: JUNI HADI AGOSTI, 2014
2.1 MATARAJIO YA
VIWANGO VYA CHINI VYA JOTO KWA MIEZI YA JUNI HADI AGOSTI 2014
Kindi cha mwezi
Juni hadi Agosti, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya
baridi katika majira haya ya kipupwe.
Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa na hali ya joto la wastani katika kipindi
cha miezi ya Juni hadi Agosti 2014 katika maeneo mengi. Aidha, izigatiwe kuwa
hali ya baridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi mapema asubuhi.
Matarajio ya viwango vya chini vya joto katika kipindi hicho ni kama ifuatavyo:
Ukanda wa ziwa Victoria (Mikoa ya Mwanza, Mara, Chato,
Kagera, Shinyanga na Simiyu)
Hali ya joto
inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu
ya nyuzi joto 17.2 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo
ya kusini ya mikoa ya Shinyanga na Simiyu hali ya joto inatarjiwa kuwa chini ya
wastani.
Ukanda wa pwani
ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, maeneo ya kaskazini ya mkoa
wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba)
Hali ya joto
inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu
ya nyuzi joto 22.9 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo,
katika maeneo ya miinuko ya mkoa wa Tanga hali ya joto inatarajiwa kuwa chini
ya wastani(Chini ya nyuzi joto 15.9 0C).
Ukanda wa nyanda
za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara)
Hali ya joto
inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati
ya nyuzi joto 13.0 0C na 15.8 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo
ya miinuko viwango vya joto vinatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 13.0 0C).
Ukanda wa
magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi)
Hali ya joto
inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto 14.9 0C na17.0
0C) katika maeneo
mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya kaskazini ya mkoa wa Kigoma (Kibondo) hali
ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Juu
ya nyuzi joto 17.0 0C).
Ukanda wa kati
(Mikoa ya Singida na Dodoma)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto14.1 0C na 14.7 0C ) katika maeneo
mengi. Hata hivyo, vipindi vya upepo mkali wenye kuambatana na baridi
vinatajiwa katika maeneo hayo.
Ukanda wa pwani
ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 19.10C) katika maeneo mengi.
Ukanda wa
kusini (Mkoa wa Ruvuma)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto
11.80C) hususan maeneo
ya magharibi mwa mkoa wa Ruvuma(Songea na mwambao wa Ziwa Nyasa). (Aidha,
viwango vya joto la wastani vinatarajiwa kwa maeneo mengine ya ukanda wa
kusini.)
Ukanda wa nyanda
za juu kusini-magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe pamoja na maeneo ya
kusini ya mkoa wa Morogoro)
Hali ya joto
inatarajiwa kuwa ya baridi kali ambapo viwango vya joto vinatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 6.00C). Hata hivyo, katika maeneo ya
kaskazini ya mkoa wa Iringa hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani.
RAMAMI INAONESHA HALI JOTO
2.2 MWELEKEO WA MVUA
KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2014
Kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti kwa kawaida
huwa ni kikavu kwa ujumla, hata hivyo vipindi vifupi vya mvua vinatarajiwa
katika maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria, nyanda za juu kaskazini mashariki na
pwani ya kaskazini . Hivyo matarajio yake ni kama ifuatavyo:
Ukanda wa ziwa Victoria (Mikoa ya
Mara na Kagera)
Vipindi vya mvua ya wastani vinatajiwa katika
maeneo hayo, hususan miezi ya Julai na Agosti 2014
Ukanda wa pwani ya kaskazini (Mikoa
ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, maeneo ya kaskazini ya mkoa wa Morogoro pamoja
na visiwa vya Unguja na Pemba)
Vipindi vya mvua za wastani vinatajiwa katika
maeneo haya, hususan mwishoni mwa mwezi Juni na katika kipindi cha miezi ya Julai na Agosti 2014
Ukanda wa nyanda za juu
kaskazini-mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara)
Vipindi vya mvua za wastani vinatajiwa katika
maeneo hayo, hususan maeo yenye miinuko na katika miezi ya Julai na Agosti
2014.
3: ATHARI NA USHAURI
Katika kipindi hicho
hali ya hewa inatarajiwa kuwa ya wastani katika maeneo mengi na vipindi vya
baridi kali katika baadhi ya maeneo. Hivyo, kwa shughuli zinazotegemea hali ya
joto wadau wanashauriwa kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana na madhara
yanayo weza kutokea kutokana hali ya hewa inayotarajiwa. Pamoja na utabiri huu
wa muda mrefu, ni muhimu pia watumiaji wakazingatia taarifa za hali ya hewa
zinazotolewa kwa vipindi vifupi.
Mamlaka inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa waendelee
kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa
wataalamu katika sekta husika.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea
kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa mrejeo kila inapobidi.
Dkt. Agnes L. Kijazi
MKURUGENZI MKUU