Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
akimkabidhi Edward Mneda nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa
kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Kati.
Kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi wa Kanda ya Ziwa Beatrice Mpanda.
Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar,
Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
akimkabidhi Rainey Mwinuka nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa
kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Ziwa.
Katikati ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera na kushoto ni
Mkuu wa Kanda Msaidizi Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi
katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha
utekelezaji wa majukumu yake.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
akimkabidhi Rainey Mwinuka nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa
kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Ziwa.
Katikati ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera na kushoto ni
Mkuu wa Kanda Msaidizi Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi
katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha
utekelezaji wa majukumu yake.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (wa
nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji mbalimbali wa
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwemo Wakuu Wapya wa Kanda
Tano za Baraza hilo muda mfupi baada ya kuzindua rasmi kanda hizo
jijini Dar es salaam. Wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk.
Primus Nkwera. Ofisi za kanda zilizozinduliwa ni Arusha (Kaskazini),
Dodoma (Kati), Mwanza (Ziwa), Mbeya (Kusini) na Zanzibar.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
(kushoto) akibadilishana mawazo na mafias wa Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi tano za kanda za
baraza hilo kwa lengo la kuharisisha utoaji huduma na usimamizi wa vyuo
vya ufundi nchini. Kanda hizo ni Kaskazini (Arusha), Kati (Dodoma), Ziwa
(Mwanza), Kusini (Mbeya) na Zanzibar.
Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi - NACTE imefungua ofisi tano za kanda ikiwa ni sehemu ya mkakati
wa wizara ya kuwekeza katika eneo la usimamizi wa sekta ya elimu nchini
ili kuongeza ufanisi na kufikia matokeo makubwa sasa (BRN).
Ofizi
hizo na makao yake makuu kwenye mabano ni Kanda ya Kaskazini (Arusha),
Kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya Kusini (Mbeya), Kanda ya Kati
(Dodoma) na Zanzibar.
Akizindua
rasmi kanda hizo JIJINI Dar es salaam mwishoni mwa wiki sanjari na
kukabidhi majukumu ya kiutendaji kwa wakuu wa kanda hizo Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome amesema
kuanzishwa kwa kanda hizo ni wazi kutaongeza ufanisi na usimamazi wa
elimu ya ufundi nchini ambayo ukuaji wake umekuwa ni wa kasi.
Profesa
Mchome amesema serikali inatambua uhitaji na mchango wa elimu ya ufundi
katika kutoa fursa kwa vijana kupata mafunzo ya stadi za kazi kwenye
fani mbalimbali na hivyo kuwezesha upatikanaji wa nguvu kazi
inayohitajika na kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri.
Amesema
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaendelea kutekeleza mikakati
iliyojiwekea ya kuhakikisha ubora wa elimu nchini unaismamiwa vema na
unalindwa hiyo ikiwa ni pamoja na kukabiliana na watoa huduma kwenye
sekta ya elimu wasiokuwa makini
"Tumeanzisha
ofisi hizi za kanda ili kuwa karibu na wadau ikiwemo wananchi na watoa
elimu ya ufundi tukiamini kuwa usimamizi wa karibu utasaidia kulinda
hadhi na ubora wa elimu ya ufundi na pia kuw ana mfumo wenye kutoa
majawabu ya haraka na kwa wakati ya changamoto pale
zinapojitokeza."Alisema Profesa Mchome
'Ni
shabaha ya serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha viwango vya
ubora wa elimu yetu katika ngazi mbalimbali unakuwa imara na wenye
kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri ili kuiwezesha sekta ya
elimu kuendelea kutoa mchango uanokusudiwa kwenye manedleoe ya kiuchumi
na kijamii kupitia rasilimali watu. Kwetu sisi hili ni jambo la msingi
na ambalo tutaendelea kuwekeza humo kulinda elimu yetu."Aliongeza
Profesa Mchome
Profesa
Mchome amesema pamoja na wizara kuwa na shabaha yake katika kuanzisha
ofisi hizo za kanda za NACTE ofisi hizo zitachangia pia kutatua
changamoto kadhaa ambazo wananchi wamekuwa wakikabiliana nazo katika
kufikia huduma kutokana na kukosekana kwa ofisi mikoani.
Amesema
utamaduni wa kutegema ofisi zilizopo makao makuu Dar es salaam unapaswa
kurekebishwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma katika sekta ya
elimu kwa ukaribu zaidi jambo ambalo litawapunguzia pia gharama
"Wizara
inatambua ,kuwa mahitaji ya wananchi kwenye taasisi za elimu ni kubwa
na hivyo itaendelea kuhamasisha taasisi zilizo chini yake kuwa na ofisi
za kanda ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa huduma."Alisema Profesa
Mchome
Katika
hatua nyengine, Profesa Mchome ameaigiza kuwa ofisi hizo za kanda za
NACTE zitumike pia kuwahudumia wadau wa elimu ya juu ikiwemo wanafuzni
wa elimu ya juu wakati Tume ya Vyuo Vikuu - TCU nayo inapojipanga
kuanzisha ofisi za kanda.
Amesema
wale wote wanaohitaji msaada na huduma na za Tume ya Vyuo Vikuu Nchini
(TCU) ikiwemo suala la uombaji udahili n.k wanaweza kufika kwenye ofisi
za Kanda za NACTE ili kupata msaada wanaouhitaji badala ya kusafiri
kwenda Dar es salaam zilipo ofisi za TCU
"Nataka
kwa wakati huu ambapo TCU inajipanga na yenyewe kuwa na ofisi mikoani,
ofisi hizi za kanda za NACTE zitumike pia kuhudumia wanafunzi wa vyuo
vikuu na wa taasisi za elimu ya juu nchini ikiwemo uombaji wa nafasi za
kujiunga na vyuo na shughuli nyengine za TCU. Ni imani yangu kwamba
agizo hili litafanyiwa kazi ili kuwaondolea wananchi usumbufu wa muda na
wa gharama wanaolazimika kufuata huduma za TCU Dar es salaam."Alisema
Profesa
Mchome amewataka wakuu walioteuliwa kuongoza ofisi hizo kuhakikisha
wanawatumikia wananchi na wadau kwa uadilifu ili lengo la Wizara la kuwa
karibu na wananchi liweze kutimia na kutoa tija inayokusudiwa.
Kwa
upadne wake Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi -
NACTE Dk Primus Nkwera amesema ofizi hizo za kanda zitakuwa na majukumu
ya kusimamia na kutekeleza mipango na mikakati ya Baraza na Wizara kwa
ujumla katika sekta ya elimu ya ufundi nchini ikiwemo udhibiti na
usimamizi wa vyuo vya elimu ya ufundi.
Aidha, Dk. Nkwera amesema ofisi hizo tayari zimeshapangiwa wkauu wake ambao wanaanza kazi mara moja
"Wadau
wote walio jirani na mikoa hiyo wanaweza kupata huduma zetu zote
pasipo kulazimika kuja Dar es Salaam. Pia waombaji wote wa programu za
shahada wanaoendelea kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao wanashauriwa
kuwasiliana na ofisi za kanda kwa kupata msaada wa haraka zaidi pale
wanapokutana na matatizo ya kiufundi."Alisema Dk. Nkwera
Kuzinduliwa
kwa ofisi hizo kunakuja wakati ambapo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi imejikita katika utekelezaji wa programu mbalimbali zenye lengo
la kufikia na kutoa matokeo makubwa chini ya mkakati mkuu wa serikali wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambapo sekta ya elimu ni moja ya sekta kuu
sita zinazopewa kipaumbele.kwenye BRN.