Msanii
maarufu na mchimbaji madini wa kampuni ya TanzaniteOne wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro
Mkoa wa Manyara, Mosses Komba (28) amenusurika kufa kwa kujipiga
risasi ya akiwa garini.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Manyara, Deusdedit Nsimeki alisema tukio hilo
lilitokea juzi saa 3:30 usiku Kazamoyo Kata ya Endiamtu.
Nsimeki alisema mchimbaji huyo wa madini ya Tanzanite alijipiga risasi ya
miguu kwa kutumia bastola yake aina ya Brown ambayo baada ya kujipiga
kwenye paja la kulia ilitokea paja la kushoto.
"Tukio hilo la kujipiga risasi limetokea kwa bahati mbaya kwani
Komba hakuiweka vizuri silaha hiyo ambayo hadi hivi sasa inashikiliwa kwenye
kituo cha polisi Mirerani baada ya baba yake kuisalimisha," alisema Nsimeki.
Alisema
bado hawajabaini chanzo halisi cha tukio hilo japo inadaiwa kuwa Komba
alichomoa bastola hiyo baada ya gari lake kugongwa ubavu wa kulia
na gari lingine ambalo halikutambulika mara moja.
Alisema
Komba alikuwa barabarani eneo la Kazamoyo akiendesha gari lake aina ya Toyota
Celica lenye namba za usajili T 725 CLK, akagongwa na gari lingine ndipo
akataka kutoa bastola hiyo ghafla ikafyetuka na kumpiga mguuni.
Nsimeki alisema majeruhi huyo Komba amelazwa kwenye hospitali ya Arusha Lutherani
Medical Center (ALMC) Seliani kwa ajili ya kupatiwa matibabu na hali yake
inaendelea kuwa vizuri.
Alisema
hadi hivi sasa hawajabaini gari lililogongana na gari la Komba ila wanawendelea
na uchunguzi wa tukio hilo huku wakiishikilia silaha hiyo na gari lake pia lipo
polisi kwa ajili ya uchunguzi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia