Waasi 100 wauawa Kordofan,Sudan
Waasi wa SPLMN wanasema ni wapiganaji watatu tu waliouawa
Jeshi nchini Sudan linasema kuwa limewaua zaidi ya waasi 100 katika jimbo la Kordofan Kusini.
Msemaji wa jeshi Sawarmi Khaled Saad anasema
kuwa mauaji hayo yalifanyika wakati wa mapigano yaliyodumu muda wa saa
tatu ya kuzima shambulizi eneo la El Atmor.
Waasi kutoka kwa kundi la (Sudanes
Peoples Liberation Movement North) walithibitisha shambulizi hilo na
kusema kuwa ni wapiganaji watatu tu waliouawa.
Kundi hilo limekuwa likiipiga vita serikali ya Khartoum eneo hilo kwa kipindi cha miaka 20 sasa
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na vita nchini humo.
Vita hivyo vimezuka wakati Rais Salva Kiir na
hasimu wake Riek Machar wa Sudan Kusini wakitarajiwa kukutana leo kwa
mazunguzmo ya amani , ukiwa mkutano wa kwanza katika kipindi cha mwezi
mmoja na wa pili tangu vita kuzuka nchini Sudan Kusini.
Mazungumzo ya kwanza kujaribu kuleta amani kati ya pande zinazohasimiana yamecheleweshwa kwa zaidi ya mara maoja.
Wajumbe kutoka pande zote wamekuwa wakikutana
katika hoteli za kifahari nchini Ethiopia tangu mwezi Januari ingawa
hakuna hatua zozote zimefikiwa za suluhu ya kudumu huku pande zote daima
zikijadili kuhusu swala tete la ajenda.
Mkataba wa kusitisha vita uliotiwa saini na Kiir
na Machar tarehe 9 mwezi Mei,umekuwa ukikiukwa na kuvunjwa na pande
zinazozozana kwenye mgogoro huo ambao tayari umesababisha vifo vya
maelfu na kuwalazimisha wengine milioni moja nukta tatu kutoroka makwao.
Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Tedros
Adhanom amesema kuwa pande zote husika kwenye mgogoro huo zimetenda
uhalifu wa kivita.
chanzo:BBC swahili
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia