Gari aina ya Toyota Vitz atakalokabidhiwa mshindi wa shindano
hilo la Nice & Lovely Miss Tanga 2014
Mratibu wa Mac D Promotions, waandaaji wa mashindano ya Nice &
Lovely Miss Tanga 2014, Benson Jackson leo amezungumza na waandishi wa vyombo
mbalimbali vya habari katika hoteli ya Mkonge jijini Tanga, ambapo
amesema mpaka sasa jumla ya washiriki 19 wamechukua na kurudisha fomu za
kushiriki shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa jiji
la Tanga, shindano ambalo litafanyika jumamosi ya tarehe 21/ 06/ 2014
Mkonge Hotel.
Shindano hilo limedhaminiwa na Nice & Lovely, EATV, Redd's, Tanga Beach Resort, Breeze Fm, CXC Africa, Rweyunga Blog na Mwambao Fm.