Meya Wa Manispaa ya Ilala Mh Jery Silaa Wa Kwanza kulia akifika eneo la Tabata St Marrys kukagua kipande cha barabara huyo ambacho kimezua mgogoro baina na Manispaa na Shirika la maji safi na salama DAWASA.
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaaa Bwana Hassan Chambuso akimuongoza Mh Meya wa manispaa ya Ilala Jery Silaa kwenda kujionea eneo la kipande cha barabara ya St Marys Tabata ambacho kinaleta shida baina ya Mkandarasi na Dawasa
Mkandarasi wa barabara ya Tabata-St Mary Bwana George Lupia wa pili kutoka kushoto akitoa ufafanuzi kwa Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa kuhusu kukwama kwake kuendelea na Ujenzi kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita Katikati ya barabara Hiyo.
Meya wa Ilala Mh Jery Silaa akifafanua Jambo kwa Mwenyekiti wa mitaa ya Tabata Bwana Chambuso kuhusu yeye Kulifuatilia Swala hilo kwenye mamlaka husika haraka iwezekanavyo,Pembeni yake ni Diwani wa Kata ya Tabata St Marys Bi Mtumwa Mohamed mwenye Dira.
Mkandarasi Geoge Lupia Akimwelezea Meya wa Ilala Mh Jery Silaa kwamba wametumia pesa nyingi katika kuchimba eneo hilo na kupata usawa wa Barabara lakini kikwazo kimekuja baada ya kukuta mabomba ya Dawasa ambayo yamekatiza katikati ya barabara na pembeni Hivyo kuleta ugumu katika kufanikisha Umaliziaji wake.
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda Akimwelezea Meya Jerry Silaa kwamba washaongea na Dawasa lakini hawapewi ushirikiano wa kutosha na wa haraka katika kushughulikia utoaji wa Mabomba hayo
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda akiendelea kufafanua jambo kwa Mh Meya wa Ilala Jerry Silaa
Meya wa Ilala Mh Jerry Silaa Akiongea na vyombo vya habari kutoa ufafanuzi wa nini kitafanyika ili kutatua mgogoro huo.
Diwani wa Kata ya Tabata -St Mary Bi Mtumwa Mohammed Akielezea ni jinsi gani wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu baada ya barabara hiyo kuchimbwa hivyo kufanya upitaji wa magari kusitishwa kwa mda eneo hilo
Mkandarasi wa barabara ya Tabata_St Marys Bwana George Lupia akiongea na vyombo vya habari kuelezea ni ugumu gani anakumbana nao katika utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo,kutokana na mabomba ya Dawasco kupita katikati ya barabara Hiyo
Hiki ndio kipande cha barabara ya Tabata-St Marys ambacho kinashindwa kuendelea na matengenezo kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita kati kati ya barabara na pembezoni,hivyo kumpa hali ngumu mkandarasi kuchimba eneo hilo ili ajaze kifusi.
Pembenini maji yaliyotuama baada ya Bomba la Dawasa kupasuka Hivyo kuleta usumbufu kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa eneo hilo.
Hilo shimo hapo ni bomba amabalo limepita katikati ya barabara
Mmiliki wa gari hii ndogo Toyota Premio alipatwa na hasira baada ya Gari yake kushindwa kupanda ili atokee upande wa pili ikambidi kushuka
Kwa hasira mmiliki huyu akatoa vizuizi ya Barabara hiyo na kuvitupa pembeni
Hapo mmiliki huyo akikagua gari yake kama imepata mikwaruzo
Wakiendelea kutazama gari yao kwa umakini
Akaamua kupanda kwa kasi baaada ya vizuizi kutolewa na yeye mwenyewe.
Meya wa Manispaaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ametembelea eneo la Tabata-St Marys kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na pia kuweza kuona mabomba ambayo yanaleta mgogoro baina ya mkandarasi na Manispaaa na Dawasa,Akiwa eneo hilo la St Marys Mh Jerry Silaa ameweza kujionea namna mabomba ya Dawasa ambavyo yamepita katikati ya barabara na pembezoni yakiwa katika kima kifupi hivyo kumzuia mkandarasi kuendelea na ujenzi wake.
Akiongea na vyombo vya habari Mh Meya Amesema kuwa barabara hiyo imetumia gharama za takribani bilioni 1 lakini imeshindwa kumalizika kwa wakati kwa sababu ndogo ya Dawasa kutokushirikiana nao ili kuweza kumpa mkandarasi ramani kamili ya bara bara hiyo,Meya Silaa akaongeza kuwa wameshawasiliana na wenzao wa Dawasa kuhusu tatizo hilo lakina wamekuwa hawapewi majibu kwa wakati na ya kuridhisha.Naye mkandarasi wa eneo hilo Bwana George Lupia amesema kuwa alipewa ramani na manispaa ambayo haikuonysha kama kuna mabomba ambayo yamepita hapo,lakini wakati ameanza kuchimba barabara hiyo ndio akakutana na mabomba hayo,Mkandarasi huyo akaongezea kwamba alishawasiliana na Dawasa kitambo sana lakini hapewi majibu ya kuridhisha kuhusu kushirikiana nao kuhamisha bomba hizo.
Naye Diwani wa kata Hiyo Bibi Mtumwa Mohhamed amesema wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu sana kwa kuwa magari yao hayawezi kutoka ndani wala kuingia kwa kuwa barabara imechimbwa kwa kina kirefu sana,hivyo amewaahidi wanainchi wa eneo Hilo kwamba wanaendelea kulitatua tatizo hilo na wenzao wa dawasco ili kuweza kuhamisha mabomba ya eneo hilo.