Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitambulisha Mhe.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa Mkuu wa Utawala na
Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka siku ya
Jumatatu June 9, 2014 Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wake
walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipo mtaa wa 22,
jijini Washington, DC.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitambulisha Mhe.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa Rais wa Jumuiya ya
Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly siku ya Jumatatu June 9, 2014 Waziri
wa Nishati na Madini na ujumbe wake walipotembelea Ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani ulipo mtaa wa 22, jijini Washington, DC.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitambulisha Mhe.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa Mwenyekiti wa tawi
la CCM DMV, Ndugu George Sebo siku ya Jumatatu June 9, 2014 Waziri wa
Nishati na Madini na ujumbe wake walipotembelea Ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani ulipo mtaa wa 22, jijini Washington, DC.
Mkuu
wa Utawala na Fedha, Mama Lily Munanka akiongea machache huku
akimshukuru Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo na
Ujumbe wake kukubali kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na
baadae kumkaribisha Balozi Liberata Mulamula kutoa maneno machache.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akiongea machache
na kumshukuru Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo na
Ujumbe wake kwa kukubali kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
na baadae kumkaribisha Mhe. Waziri kuongea machache na Maafisa, na
Wafanyakazi wa Ubalozi huo wakiwemo wanajumuiya.
Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akiongea
machache na kumshukuru Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa makaribisho
mazuri na kuelezea sababu ya ujio wake nchini Marekani ambao alianzia
New York kwenye mkutano wa mwongo wa Nishati Endelevu kwa wote (SE4ALL) ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, siku ya alhamisi wiki iliyopita aliuzindua
rasmi mkutano uliohudhuriwa na wajumbe zaidi wa 1,000 wakiwamo
zaidi ya mawaziri 20 wa Nishati, wafanyabishara, mashirika ya kimataifa
yakiwamo ya fedha na Asasi zisizokuwa za kiserikali,
Ujumbe
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu ambao ulianza
Juni 4 na kumalizikaJuni 6, uliongozwa na Waziri wa Nishani na Madini
Professor Sospeter Muhongo ambaye pamoja na kuhudhuria na kuchangia
mijadala mbalimbali, ijumaa ( June 6), alizungumza katika mkutano
wa mawaziri kuhusu nafasi ya Nishati katika Ajenda za Maendeleo
Endelevu baada ya 2015 na utayari
wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Bara la Afrika kuhushu Nishati
Endelevu kwa wote unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.
Picha ya pamoja ya Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula.
Waheshimiwa Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi
Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Maafisa na Wafanyakazi wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Waheshimiwa Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi
Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Ujumbe aliokuja nao Mhe.
Waziri wa Nishati na Madini kutoka kushoto ni Eng.Jones Olotu(Rural
Energy Agency wa Wizara ya Nishati na Madini), Eng. Rwatabangi P.
Luteganya (Manager Investment TANESCO), Styden Rwebangila (Energy
Engineer Wizara ya Nishati na Madini), Venosa Ngowi (Senior Petroleum
Geologist TPDC), Eng. Leonard R. Masanja (Director TANESCO Board of
Directors) na Eng. Yahaya I. Samamba (private Secretary to Minister
Wizara ya Nishati na Madini)
Waheshimiwa Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi
Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Wanajumuiya DMV
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia