WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUSHIRIKIANA NA TMF ILI KUPUNGUZA UTEGEMEZI WA MATANGAZO
Waziri
wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa
wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari
kwenye maeneo matano, sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia,
kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya
Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa
vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa
Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa
Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.(Picha zote na Zainul Mzige).
Na Damas Makangale
WAANDISHI
WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo
vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna
weka taaluma yao rehani.
Akizungumza
na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa
waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji,
unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya na
watayarishaji wa vipindi vya luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe,
Gaudensia Kabaka amesema kwamba vyombo vya habari lazima vishirikiane na
mfuko huo ili kuwa huru wakati wa kuripoti.
“kuendelea
kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha
kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa
ujumla,” amesema Kabaka
Amesema
mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa
sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa
kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za
kulevya.
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani.
Kabaka
aliongeza kuwa mafunzo haya yatakayotolewa kwa ufadhili wa TMF ni
muhimu ili kuelimisha jamii madhara ya kuuza na kusambaza dawa za
kulevya na matumizi yake yanavyoathiri kizazi na kizazi.
“kwa
sasa nchi yetu ya Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na
matumizi ya dawa za kulevya na mbaya zaidi kutumika katika njia ya
kusambaza madawa hayo hatari,”
“kwa
mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tuna jumla ya watu 20,626
walioathirika na dawa za kulevya na kwa sasa wanapatiwa matibabu,”
alisisitiza Kabaka.
Amesema
nchini matumizi ya dawa za kulevya kwa zaidi ni Bangi, Heroin, Mirungi
na Cocaine na cha kutisha matumizi haya yanaathiri pia wanafunzi wa
sekondari na shule za msingi nchini.
Msaidizi
wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu(UNFPA),
Dorothy Temu Usiri akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo uliofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Kwa
upande wake, Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa
wa Idadi ya watu, Dorothy Temu-Usiri amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo
vya kikatili vya kijinsia na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
vimechochea kushirikiana na TMF kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari
hapa nchini.
“kwa
kuanzisha mafunzo haya ya bure kutasaidia waandishi wa habari kuandika
kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndio
kichocheo cha ukatili wa kijinsia hasa kwa Wanawake,” amesema Usiri.
Usiri
aliongeza kwamba nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wenye nguvu ya
kufanya kazi ni vijana kwahiyo ni muhimu jamii ya kimataifa kushirikiana
na serikali na taasisi zingine ili kunusuru kundi hili muhimu kwenye
nchi.
Mkurugenzi
wa TMF nchini, Ernest Sungura akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi
huo wa mafunzo ya bure yanayofadhiliwa na mfuko wake ambapo amesema
kwamba malipo madogo kwa wahariri na waandishi wa habari kunadidimiza
taaluma ya uandishi wa habari pamoja na swala la kutokubobea katika
sekta husika (Specialization).
Wadau
watakaoshiriki kwa ukaribu kwenye mradi huo wakitambulishwa kwa mgeni
rasmi kutoka kushoto ni Dkt. Pilly Said kutoka kitengo cha madawa ya
kulevya hospitali ya Mwananyamala, January Nzisi Mkuu wa Kitengo cha
Mtandao Tume ya Kudhibiti Madawa ya kulevya, Geodfrey Nzowa, Kamishina
Msaidizi wa Jeshi la Polisi, kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya,
Bi. Aida Teshe Kaimu Kamishina kutoka Tume ya Kudhibiti Madawa ya
Kulevya (DCC) na Florence Bahati Khambi Afisa Habari kutoka Tume ya
Kudhibiti dawa za kulevya.
Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia yaliyojiri kwenye uzinduzi
wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo
matano, viwanda, jinsia, madawa ya kulevya, kuzuia madawa ya kulevya kwa
waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya
luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Afisa
Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella
Vuzo amesema kwamba mradi huo umekuja katika muda mwafaka kwa taifa la
Tanzania kwa sababu takwimu za matumizi ya dawa za kulevya zinatisha kwa
vijana ni lazima taasisi za ndani na jamii za kimataifa kushirikiana
kupambana na janga hili.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali.
Afisa
Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella
Vuzo (kulia) pamoja na Bw. Phillip Musiba kutoka UNIC.
Afisa mafunzo wa TMF, Bi. Raziah Mwawanga akinakili mambo muhimu yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA(Mstaafu) Ananilea Nkya (kushoto) na Mwandishi wa
Habari Mkongwe Mama Eda Sanga (katikati) ambaye ni miongoni mwa mentors
kwenye mradi huo. Kulia Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.