WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili
tofauti likiwemo la mfanyabiashara wa madini kupigwa risasi na watu
wanaosaidikiwa kuwa ni majambazi katika
eneo la Maeda lililopo ndani ya
halmashauri ya jiji la Arusha.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa
wa Arusha SACP Leberatus sabas alisema kuwa katika tukio la kwanza lilitokea
mapema June moja majira ya saa 9:15
katika endoe la mtaa wa maenad ambapo mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la
Benedict Gabriel mwenye umri wa miaka 58 mfaya biashara wa madini na mkazi wa
Mushono alifariki dunia mara kupigwa risasi .
Alisema kuwa tukio
hilo la kupigwa risasi kwa
mfanyabiashara huyu wa madili lilitokea wakati marehemu Benedict Gabriel kutaka kutoa msaada kwa Monica Msuya (47) mkazi wa Mbauda mfanya biashara wa Northern
Bereau de change ambapo alikuwa
akivamiwa na majambazi hao na kumpora mkoba ambao ulikuwa na shilingi
5,000,000 na kukimbilia pasipojulikana
Sabas alibainisha
kuwa uchunguzi wa awali onaonyesha kuwa
monica Msuya alitokea katika hotel ya
Impala kuchukuwa pesa hizo
na kuelekea kazini akiwa amepanda tax ambapo mara baada ya kushuka
nakufungua mlango wa kuingia ofisini kwa
gafla alitokea kijana mmoja na kutaka
kumnyanganya mkoba ndipo alipoanza
kupambana nae lakini kijana huyo alimpiga monika msuya makofi mawili na kumpiga
ngwara kasha kuangaka chini ndipo monika alipo piga kelele na kuomba
msaada huku akiwa ameshikilia mkoaba
wake wenye
“wakati sasa anapiga kelele marehemu Benedict Gabriel
alijitokeza nakuanza kutoa msaada na kijana mwingine aliyebaki kwenye pikipiki alitoa bunduki aina ya Shortgun na kumlenga marehemu ,ambapo
mara baada ya kumpiga marehemu aliaanguka
na Yule kinana alifanikiwa
kuchukuwa mkoba ule na kukimbia
wakiwa na pikipiki aina ya toyo yenye rangi nyekundu akiwa na mwenzake aliyekuwa anaendesha toyo
ile “alisema Sabas
Wakati huo huo gari aina ya nissani minibus lenye namba za
usajili T. 319 AXT imemgonga mtembea kwa miguu ambaye ni askari polisi
aliyefahamika kw a namba E.5921 CPL Justine (43) katika eneo la
ngarenaro jijini hapa .
Kamanda wa polisi mkoani hapa amedhibitisha kutokea kwa ajali
hiyo ambapo alisema kuwa miili yote ya marehemu imeifadhiwa katika katika
hospitali yamkoa ya maunti meru ,huku akibainisha kuwa jeshi la polisi
linaendea kuwasaka majambazi waliousika na mauaji ya Benedict Gabriel.
Adha kamanda wa polisi alitoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya
usafiri na watembea kwa miguu kuwa
makini wakiwa katika barabara ili
kuepuka na ajali za mara kwa mara.