ADY BATISTA WA “THE THORN OF THE ROSE” AKONGA NYOYO ZA WAPENZI WA SINEMA TAMASHA LA ZIFF 2014

DSC_0128
ADY de Batista (30).
DSC_0154
ADY de Batista akisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta mara baada ya kuwasili kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
ADY de Batista alishuka taratibu katika gari la Noah, akiwa amevalia nguo nyeupe.Alisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta na kuingia katika ukumbi wa maonesho ya sinema wa wazi uliopo Ngome Kongwe kwa ajili ya sinema yake ya O Espinho Da Rosa.
Kutoka kwenye gari hadi alipopokewa na Mtendaji wa tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) Profesa Martin Mhando,unamuona mdada anayejiamini, mwenye uzuri wa asili na weusi unaong'aa majira ya magharibi kabisa, kabla ya swala ya insha.
DSC_0157
ADY de Batista akiingia kwenye lango kuu la Ngome Kongwe.
Alikuwa anatembea taratibu kama malkia kushoto akiwawepo meneja Sholey na Kulia rafiki yake wa kiume Antoine Simonet.Nyuma alikuwapo mdogo wake Nautenle Batista.
Alipokewa na Mtendaji wa ZIFF Profesa Martin Mhando ambaye alizungumza kidogo kuhusu O Espinho Da Rosa (The Thorn Of The Rose) kabla ya kumkaribisha kuzungumza na wapenzi wa sinema waliokuwa wamejazana pomoni katika ukumbi wa sinema.
DSC_0181
ADY de Batista na Meneja wake wakielekea kwenye jukwaa la ZIFF 2014 kuhutubia.
Kabla ya kuzungumza kuhusu filamu hiyo ambayo imechezwa na Júlio Mesquita, mwenyewe Ady Batista, Daniel Martinho, Ângelo Torres na Ciomara Morais, Ady alishukuru kuwepo Zanzibar na kusema kwamba ndoto yake imetimia, anashukuru sana.
Sinema hii ambayo ni saa moja na dakika 37, ni sinema yenye makali yote ya maisha, mashaka na pia imani zilizojikita vyema katika jamii ambayo imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali.
DSC_0194
ADY de Batista akizungumzia filamu yake.
Maneno ya ndoto kutimia yameonesha furaha aliyoiandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook Mei mwaka huu baada ya kuambiwa kwamba filamu yake imeingia katika mashindano ZIFF.
Katika hiyo face book ya Mei mwaka huu aliandika: E nós fomos seleccionados! Júlio Mesquita Audilia Batista Daniel Martinho Daniel Martinho Angelo Torres Ciomara Morais Sonia Claudia Neves Eric Santos Eric Santos akimaananisha : Tumechaguliwa! akiwataarifu Júlio Mesquita Audilia Batista Daniel Martin Daniel Martin Angelo Torres Noelle Matthews Sonia Santos Santos Eric Eric Claudia Neves .
DSC_0186
Shangilio lililokuwa katika facebook ndilo hasa alilolionesha wakati akizungumzia sinema yake hiyo ambayo ilipigwa picha kwa siku 20 na kutoa matokeo kama sinema ya Hollywood kwa ubora.
Ikiwa inajulikana kama The Thorn of the Rose,kwa kingereza, filamu hii ambayo ilikuwa ya kwanza kwa mtengeneza sinema Filipe Henriques ipo katika maelezo ya ushindani ambayo yanatoa ubora wa picha na skripti yenyewe kwa namna ambavyo matukio yamefungwa pamoja na kuwa kama visa zaidi ya viwili katika filamu.
DSC_0207
Kiukweli wakati natazama sinema hii Ngome Kongwe na hata katika maonesho binafsi ya ndani ya ukumbi wa kujitegemea Double Tree Hotel, ina wakati inakuchanganya mwenendo ambao unatakiwa kuwa nao makini kwani kuna muda unajisikia kama kutapika kwa hasira wakati mtengeneza sinema alipokuwa akiiperemba jamii na makovu ya wanasiasa.
Unaweza kusema kwamba simulizi hili lina mashetani, lakini masimulzii yake yanakupa neno jema kabisa la kuzungumza wakati ukimaliza kuona sinema hii.
Mwendesha mashtaka David Lungha (Júlio Mesquita) katika filamu hii anakutana na binti mrembo ambaye uwepo na utokeaji wake ni wa 'utata' zaidi anayekwenda kwa jina la Rosa (Ady Batista).
Hawa wawili wanakutana katika baa ambapo watu walikuwa wanamsubiri kumpa hongera kwa ushindi wake mahakamani. Amabo anaukiri na kusema mapambano yanaendelea.
Akisema hivyo anakwenda kukaa katika kiti cha baa na pembeni mwake kuna askari polisi.
Akiketi pale mmoja wa wasaidizi wake anafika kwake akionekana wazi si tu kutoa hongera bali kumtaka kimapenzi na kumkataa, lakini akiondoka analetewa bahasha na mtandia , lakini kabla ya hapo anazungumza na polisi ambaye anamwambia hakuna ua waridi lisilokuwa na miba na ogopa unapopata ua waridi tatu.
Akaondoka akmfyonza lakini kweli aliona kuna ua waridi na maneno ya polisi yanaweza kuwa kweli.
DSC_0230
Muda mfupi tunasikia kishindo cha kiatu na anaingia binti wa kike ambaye mwendesha mashtaka anaingiwa na kwikwi na wanaanza mambo ambayo yanapeleka katika mtandao mkubwa zaidi wa uwongo, kusalitiana, mauaji na rushwa.
Ukiangalia sinema hii hata mwanzo unapata maswali mengi kama kweli Rosa ni mtu kweli au ni mawazo ya mwendesha mashtaka, ama ni mzimu ambao hauwezi kutulia kuzimu mpaka habari ya kifo chake ielezwe.
katika simulizi hili muigizaji kinara David Lungha ni mwanamume mwenye mvuto mkubwa wa kimapenzi lakini mtata; na mtu wetu wa leo katika sebule la sinema Ady Batista ni mdada mzuri, ambaye anaonekana kuchukua kiatu cha Rosa, kama asiyekuwa na raha huko aliko.
Ndani humu Eric Santos ni askari ambaye amekuwa polisi akiwa na siri nyingi mbaya za kwake.
Lakini msimuliaji wetu anataka kukueleza kwamba si sahihi kuacha kurekebisha mambo na wale waliokufa, kwani hutafuta njia ya kurudi na kurekebisha mambo yao, imani ambayo Waguinea wanayo sana.
Mapenzi ya mwendesha mashtaka David Lunga kwa Rosa kuna vuruga kila kitu na Lunga anajikuta akifanya vitu vingi kwanza kumaananisha kwamba hana kosa wala hana sababu ya kujuta.
DSC_0248
Filamu hii ambayo iliwapa shida watu wa sensa wa ZIFF ili iweze kuonwa na watu wengi ukumbi wa wazi, unazungumzia kwa namna ya pekee rushwa, ubakaji ambao unafanywa katika maisha ya binti, kifo chake na jinsi ambavyo anataka jumuiya ijue.
Pamoja na kwamba binti alikufa katika utata wa kutoa mimba alirejea duniani kutafuta msaada wa haki kutendeka na katika hili Polisi yule (askari wa zamani) aliwaua lakini akashindwa kummaliza moja kwa moja Lunga ambaye alimuua.
Kiukweli kuelekea mwisho wa sinema unaona matukio mengi na jinsi hali ilivyo ngumu na lazima aifanyie kazi.
Filipe Henriques ameifanyakazi kubwa sinema hii ambayo imejaa usaliti kuanzia wa kisiasa, kijamii hadi kimapenzi huku mazungumzo yakiwa mapenzi kwa watoto wadogo.
Lugha ya kireno ambayo imeambatana na lugha ya kiingereza katika maandishi yanayopita si nzuri kihivyo, lugha ina matusi mengi na isiyopendeza na kuna grafiki za mapenzi ya kulazimishwa katika hali isiyokubalika.
DSC_0249
ADY de Batista akiondoka mara baada ya kumalizika kwa filamu yake.
Mdada huyu ambaye katika mazungumzo alisema kwamba simulizi la sinema ile ni matukio ya kweli nyumbani kwao ambapo pia kuna imani kubwa kuhusu mizimu kurejea duniani pamoja na kuwapo dini ya Kikristo na Kiislamu,ametaka jamii kujipambanua na maradhi ya woga na kuchukua hatua kwanza binafsi na kisha kijamii dhidi ya maovu.
Mdada huyu ambaye hajaolewa lakini ana rafiki wa kiume, alikuwa Zanzibar na mdogo wake na Meneja wake.
Mdogo wake ndiye anayejua kiingereza kwa ufasaha zaidi huku yeye mwenyewe amebahatisha.
Nilipomuuliza kuhusu nguo yake nyeupe, kwani katika sinema kuna vazi la harusi, alisema rangi nyeupe ni alama ya matumaini.
DSC_0257
Kuendelea kusoma zaidi bofya hapa

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post