Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram
wamewateka nyara wanawake 20 kutoka jamii inayohamahama Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria.
Wanawake hao walichukuliwa katika Makazi ya
Gakini Fulani karibu na mji wa Chibok ambako zaidi ya wasichana
wanafunzi 200 walitekwa nyara Aprili, mwaka huu.
Walioshuhudia tukio hilo walisema
kuwa wapiganaji hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwalazimisha
wanawake hao kuingia katika magari yao kabla ya kutoroka nao katika
Jimbo la Borno.
Mlinzi mmoja wa kijiji alisema kuwa washambulizi
hao pia waliwateka nyara wanaume watatu waliojaribu kuwazuia wasiondoke
na wanawake hao.
Hadi sasa jeshi halijasema lo lote kuhusiana na tukio hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Chibok
ambako wapiganaji wengine wa silaha waliwteka nyara zaidi ya wasichana
200 wanafunzi Aprili, mwaka huu.
Wakati huo jeshi la Nigeria limesema kuwa
limewaua wapiganaji 50 katika kampeni yake dhidi ya magaidi mwishoni mwa
wiki katika majimbo la Borno na Aladawa.
Mfululizo wa mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo umeimarisha ukosoaji wa vyombo vya usalama vya Serikali.
Licha ya kuwepo kwa hali ya hatari katika eneo
la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wanajeshi hawajachukua hatua dhabiti
na wakati mwingine hawapo wakati washambulizi wanaotekeleza uhalifu wao.
chanzo: BBC swahili
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia