Faili la tuhuma dhidi ya
Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.
Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.
“Tuhuma dhidi yangu ni za kutengeneza,” alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku kadhaa.
“Mimi sijabaka na sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu atanitetea,” alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.
“Si wamesema wananitafuta, nitakwenda mwenyewe polisi. Nitawasikiliza na nitatoa maelezo yangu. Kama wakinipeleka mahakamani basi ukweli utajulikana… ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.”
Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari kung’amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).
Kadhalika binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.
Akiwa nje ya kituo cha polisi Jumatatu usiku, binti huyo aliliambia gazeti hili kwamba mara ya kwanza alibakwa mchana Mei 23 na kwamba mtuhumiwa alirudia kitendo hicho Jumapili Mei 25 usiku ndani ya gari katika eneo la Tabata, ambako anadai alifanyiwa kitendo hicho mara mbili.
Hata hivyo, Mbasha alihoji: “Hivi kweli hata kama mimi ni mbakaji, kweli nimbake mtoto wa kumlea mwenyewe mara tatu, yaani Ijumaa halafu nirudie tena Jumapili? Hata kama ni kusingiziwa basi tuhuma hizi zimezidi.”
“Huyu binti nimekaa naye miaka mingi na sijawahi kumfanyia hivyo. Hapo nyumbani kwangu wamekaa mabinti wengi, wakiwamo shemeji zangu wadogo zake na Flora na sikuwahi hata kuwagusa, leo hii kwa nini wananifanyia hivi?”
Mgogoro wa familia
Mbasha alidai kwamba chanzo cha kusingiziwa kwake ni mgogoro baina yake na mkewe Flora, ambao umesababisha mgawanyiko mkubwa ambao umefanya achukiwe na familia nzima ya mkewe.
“Yako mambo mengi tu ambayo yanahusu familia, kwa hiyo ilifika mahali mimi na Flora tukawa hatuishi kwa amani na hata hili jambo limetokea wakati tukiwa na mgogoro huo. Hivyo Flora na ndugu zake waliamua kumlisha binti huyo maneno ili mimi nifungwe,” alisema Mbasha.
Hata hivyo, Flora hakutaka kuingia kwa undani katika suala hilo, akisisitiza kuwa Mbasha bado ni mumewe na kwamba yaliyotokea awali alishamsamehe, lakini akamtaka ajitokeze kutoa maelezo polisi.
“Mimi nilishamwambia kwamba hata kama alifanya au hakufanya, nilishamsamehe kutoka ndani ya moyo wangu maana yeye ni mume wangu wa ndoa na Mungu wangu ni shahidi, lakini kuna suala la kisheria polisi ambalo mimi siwezi kuliingilia,” alisema Flora ambaye alitamba na wimbo wa injili wa “Tanzania” ambao ulimfanya aalikwe katika shughuli mbalimba za kitaifa.
“Tatizo linakuwa kubwa kwa sababu yeye mwenyewe haonekani na taarifa ni kwamba amekimbia,” alidai Flora. “Sasa kama kweli hajafanya kitendo hicho, kwa nini anajificha? Ajitokeze… aende polisi na huko ndiko akatoe maelezo yake. Kuzungumza na vyombo vya habari haisaidii kabisa.”
Mwimbaji huyo, ambaye ni mjukuuu wa muhibiri maarufu wa Injili, Askofu Moses Kulola alisema yeye hana uwezo wa kuingilia kesi hiyo kwani hakuhusika kwa namna yoyote ile kupeleka suala hilo polisi kwa sababu hakuwapo wakati likitokea na kwamba linasimamiwa na familia.
“Inawezekana anatamani nikafute kesi polisi, mimi sina uwezo huo kwa sababu ni suala la kisheria na tuhuma zenyewe ni za kijinai. Pili familia yenye mtoto ndiyo inafuatilia kesi hiyo, lakini hilo halifuti msamaha wangu kwake,” alisisitiza.
Kauli ya Flora kwamba ameshamsamehe mumewe inafanana na ya Mbasha ambaye pia alisema kwamba kama kuna jambo ambalo mkewe alimkosea, hana tatizo na kwamba alishamsamehe.
“Flora ni mke wangu, mke wa ujana wangu, ninampenda asilimia 100 na yeye analifahamu hilo, lakini sijui ni kitu gani kimemkuta? Sijui ni nini kimeingilia ndoa yetu?” alisema Mbasha.
Alisema ameshampigia simu mkewe mara nne akitaka waonane ili wazungumze, lakini hakuonyesha utayari, kauli ambayo Flora aliikanusha akisema: “Hajanitafuta maana tangu Jumatatu hapatikani kwenye simu.”
Mwenendo wa upelelezi
Wakati hayo yakiendelea, maendeleon ya kesi hiyo yanasuasua baada ya faili kutokupelekwa Kituo cha Polisi Buguruni kutoka Tabata kwa ajili ya hatua zaidi.
Baadhi ya wanafamilia wa mtoto anayedaiwa kubakwa walisema jalada hilo lingefikishwa Buguruni Jumatano jioni, lakini kutokana na ofisa anayeshughulikia kesi hiyo kuwa na udhuru, ilishindikana.
Mjomba wa Flora ambaye amepewa jukumu la kusimamia kesi hiyo, alisema wamekuwa wakifuatilia Kituo cha Polisi cha Tabata tangu tukio hilo liliporipotiwa, lakini wakaelezwa kuwa kesi hiyo itahamishiwa Buguruni.
“Tuliambiwa lile faili lazima lihamie kituo cha Buguruni. Nilifika hapa nikaonana na kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ametupokea vizuri na kuonyesha moyo wa kutusaidia,” alisema.
Kamanda wa polisi wa Ilala, Marietha Minangi alisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kesi hiyo na kwamba hafahamu taarifa kuwa faili hilo linacheleweshwa kuhamishiwa Buguruni. “Tunaendelea kuchunguza, ila siyajui hayo masuala ya faili yanayotoka kinywani mwako. Lakini nimepata taarifa kuwa bado wanachunguza,” alisema Minangi.
Mwanzoni mwa wiki jana, Kamanda Minangi alisema kuwa maofisa wake walikuwa wanaendelea kumsaka mtuhumiwa na kwamba walienda mpaka nyumbani kwake, lakini hawakumkuta.
“Nimefuatilia ni kweli hiyo kesi imefunguliwa na maofisa wangu wameniambia walienda nyumbani kwake na hawakumkuta mtu. Waliniambia walikaa pale kwa takribani dakika 20 na ile nyumba ina fence (uzio) na geti waligonga kengele, lakini hakuna mtu aliyekuja kufungua.
“Na baadaye waliwauliza majirani, nao wakasema hawafahamu mtu huyo alipo. Inaonekana ametoweka, lakini sisi kama wasimamizi wa sheria tunaendelea kumtafuta mpaka tutakapomkamata,” alisema Minangi.
Ustawi wa Jamii
Kesi hiyo pia inafuatiliwa kwa karibu na Idara ya Ustawi wa Jamii ya Manispaa ya Ilala kujua usalama na matibabu ya binti huyo. Ofisa ustawi wa jamii anayeshughulikia ulinzi na usalama kwa mtoto wa manispaa hiyo, Fransica Makoye alisema kuwa wanalishughulikia suala hilo kama mengine katika kutafuta haki na usalama wa mtoto na wala hawahusishi na umaarufu wa wahusika.
“Sisi tunafuatilia kama alipata tiba sahihi mara baada ya tukio la kubakwa na kufahamu mahali ambako anakaa kwa ajili ya usalama wa huyo mtoto. Tumeiona PF3 haionyeshi kama alipata matibabu, lakini tutawajulisha zaidi kinachojiri kwa kuwa tutaenda Hospitali ya Amana kwa maelezo zaidi,” alisema Makoye.