Vijana na Watanzania kwa jumla wameaswa kuacha kutegemea ajira za
ofisini, badala yake watafakari namna ya kujiingiza katika ujasiriamali
ili kuondokana na umaskini.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitivo cha Elimu
ya Biashara na Uchumi wa Chuo Kikuu cha Iringa (IUCo), Enock Ugulumo
wakati alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya ujasiriamali
iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho mjini Iringa.
Maadhimisho hayo yalilenga kuwaongezea vijana na
wanafunzi wa chuo hicho maarifa katika kujitegemea. Utafiti wa wataalamu
mbalimbali duniani unaonyesha asilimia kubwa ya watu wanaogemea ajira
hufa wakiwa maskini, tofauti na wale wanaojiajiri.
Alisema chuo hicho kimeanzisha mpango huo
chuoni hapo ili kuibua vipawa vya vijana na kuwawezesha wanafunzi
kutumia elimu na ujuzi walionao kuibua ajira mpya, hatua itakayotoa
fursa kwa jamii kupata nafuu ya upatikanaji wa kazi.
“Mfumo huu wa ujasiriamali ambao unaendana na
mafunzo kwa vitendo, umelenga kuwafundisha wanafunzi namna ya
kutengeneza bidhaa na kutoa huduma, kama sehemu ya kukabiliana na tatizo
la ajira”.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha
Ujasiriamali wa Chuo hicho Dk Hosea Mpogole alisema mpango wa
ujasiriamali kwa wanafunzi ulioanzishwa chuoni hapo utapunguza kero ya
upatikanaji wa ajira nchini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia