baadhi ya warembo wanaogombania ulibwende wa mkoa wa manyara
warembo wa redd's miss manyara wakiwa wanacheza ikiwani moja ya mazoezi
Kinyanganyiro cha
kugombea Redd’s Miss Manyara 2014, kinatarajia kufanyika Juni 14 mwaka huu
katika ukumbi wa CCM Mkoa, mjini Babati, ambapo warembo kumi wanatarajia
kuchuana.
Mkurugenzi wa Mirerani Entertainment, Akon Clement ambaye ni Mratibu wa mashindano hayo alisema mgeni rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mary Nagu.
Akon alisema msanii
maarufu wa kizazi kipya, Bob Junior kutoka jijini Dar es salaam anatarajiwa
kutoa burudani kali wakati akisindikiza michuano hiyo ambapo pia wasanii
chipukizi kutoka mjini Babati watashiriki kunogesha.
Aliwataja wanyange
hao wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kuwa ni Miss Mirerani 2014 Amina
Omary, Miss Mirerani namba mbili Catherine Emmanuel na Miss Mirerani namba tatu
Happy William.
“Wengine ni Fatuma Salim, Betha Fredrick, Rose Evason,
Edna Mushi, Hosiana John, Mary Ruta na Flora Godlizen, ambao ni warembo
walioshinda kwenye mashindano ya wilaya za Babati, Hanang’ na Mbulu,” alisema
Clement.
Aliwataja wadhamini
wa mashindano hayo ni kampuni ya Tanzania Breweries (TBL), kupitia kinywaji
chake cha Redd’s Original, Open University, Manyara Computer,
mireranitanzanite.blogspot.com na Active Classic Fashion.
Mratibu huyo alisema
kuwa wadhamini wengine wa shindano hilo ni TanzaniteOne, Assey Printing
company, Trimus Saloon, Kifaru Agrovet, Winners Hotel, Sarafina Lodge na
Kimweri Sport Wear.