Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akioneshwa vipande vya madini aina
ya Tanzanite ,katika mgodi wa mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite
Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM alitembelea migodi ya
wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto
zinazowakabili na namna ya kuzitatua. Pichani kati aneshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Christopher Ole Sendeka.
Moja ya jiwe lenye madini kabla ya kufanyiwa mchakato.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia namna wachimbaji wadogo
wanavyotumia mashine kubebea mchanga kutoka kwenye mgodi wa mchimbaji
mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM
alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao
juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mererani
ambao aliwaambia vyama vya Upinzania ni sawa na Jogoo kwani hata awike
vipi hawezi fungua mlango na kwa sababu vyama hivyo havipo kwa ajili ya
maendeleo ya wananchi basi vinelekea kufa kwani havina sera mpya za
kujinadi kwa wananchi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mererani
wilaya ya Simanjiro ambao wengi ni wachimbaj wa wadogo wadogo wa madini
kwenye mkutano wake wa mwisho baada ya kumaliza ziara ya siku 26 ambapo
alitembelea mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara.
Jengo
la Kituo cha Afya cha Endiamtu,Mererani Simanjiro,ambapo Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana alikwenda kukagua na kujionea ujenzi wake ulipofikia
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha
afya cha Mama na Matoto cha Endiamtu,Mererani wilayani Simanjiro.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa tanki
la maji litakaloweza kuhudumia watu 25,000 na kutoa lita 36,000 kwa saa
linalojengwa Naisinyai Mererani.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Landanai,Wilayani Simanjiro
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Landanai,Wilayani Simanjiro
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiri ujenzi wa Ofisi ya tawi jipya la CCM la Kandasikira.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya Chama Cha
Mapinduzi baada ya kuzindua tawi jipya la CCM tawi la Kandasikira.
Baadhi
ya Wazee wa Kimasai wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
alipofanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kandasikira,Wilayani
Simanjiro.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kandasikira,Wilayani Simanjiro.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kandasikira,Wilayani Simanjiro.