INNOCENT NGANYAGWA KUTUMBUIZA TAMASHA LA ZIFF 2014 USIKU HUU NDANI YA UKUMBI WA MAMBO CLUB, NGOME KONGWE

DSC_0276
Mwanamuziki Mkongwe wa Rege nchini, Innocent Nganyagwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na show yake kwenye tamasha la ZIFF 2014 usiku wa leo ndani ya ukumbi wa Mambo Club kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.Kushoto Mtaalamu wa masuala ya habari ZIFF, Bw. Dave Ojay.
DSC_0094
Baadhi ya wageni mbalimbali na waandishi wa habari wanaohuduria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar.
Na. Mwandishi wetu.
BAADA ya kutoa demo katika mkutano wake na waandishi wa habari, mkali wa rege nchini Innocent Nganyagwa ameahidi kuporomosha muziki mzito katika ukumbi wa mambo klabu leo usiku.
Katika demo ambapo alipiga verse ya gila, mkali huyo aliwataka wazanzibari kuingia kwa wingi kuona sweet reggae baada ya mfumo wa Babylion wa ukombozi kumalizika.
Anasema kwamba wapenzi wake watarajie vitu vipya kuonesha kwamba yeye hajalala kwa miaka yote hata baada ya kuonekana kuwa nje kwa miaka 9.
Nganygwa mwenye tuzo tano za nyumbani na albamu nne katika mikono amesema kwamba kimya chake kilitokana nba kuamua kusuka kizazi kipya cha rege kupitia kampuni yake ya Reggae Production.
Akizungumza kuhusu muziki wake alisema kwamba yeye anapiga muziki wa rege lakini si kwa mtazamo wa Jimmy Clief,Bob marley na Burning Spear ; ni muziki wenye utamaduni wa nyumbani na hivyo kwua na rege yenye utambulisho wa Tanzania.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post