Mkurugenzi wa TAHA,
Bi Jacqueline Mkindi akiwa anawaelezea waandishi wa habari nia haswa ya wao kama taha kushiriki kuandaa maonyesho haya
Tanzania Tanzania Horticultural Association
(TAHA) kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo
(SIDO) wameandaa maonyesho ya siku sita kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi
pamoja na wajasiriamali jinsi ya kuzifanya bidhaa zao kuwa na ubora wa
kimataifa.
Akiongea leo na waandishi wa habari meneja
wa shirika la SIDO Isdori Kiyenze alisema kuwa maonyesho hayo yanatarajiwa kuanza rasmi
tarehe saba hadi kumi na mbili ambapo
alibainisha kuwa yanatarajiwa kufunguliwa june 9 na waziri wa viwanda na
biashara Abudala kigoda katika viwanja vya makumbusho vilivyopo jijini hapa.
Alisema kuwa nia haswa ya kuandaa maonyesho
haya nikuwajengea uwezo mkubwa
wajasiriamali wadogo wadogo na kuwafundisha namna mbalimbali za kisasa za kutengeneza bidhaa
zao na kuzihifadhi (kuparki) katika hali nzuri ya kimataifa ikiwa ni pamoja na
kusindika .
Alisema kuwa pia watatoa mafunzo mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuwafundisha teknoligia
mbalimbali za kisasa zinazofanya kazi katika kipindi hichi.
“unajua
wajasirimali wetu wengi wamekuwa wanatengeneza vitu vizuri na vyenye ubora ambavyo avina tofauti
na vya nchi zingine lakini vimekuwa
avithaminiwi sasa sisi kama sido tumepita katika supermarket mbalimbali
tumeangalia vitu vilivyosindikwa tukaona sasa havina tofauti na vitu vyetu
ambavyo tunalima tukaamua kuwapa elimu wajasirimali wetu sasa kunawengine ambao
hawakupata elimu ndo tunataka tuwape katika kipindi hichi cha maonyesho haya”alisema
Kiyenze
Kwa upande wa Mkurugenzi wa TAHA, Bi
Jacqueline Mkindi alisema kuwa wao kama
taha wameamua kushirikiana na sido kuandaa maonyesho haya ili kuweza kuwajengea
uwezo zaidi wajasirimali wadogowadogo .
Alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakiweka
nguvu zao nyingi kwa wazalishaji lakini
kwa sasa wameamua kungia na huku ili kuweza kuwasaidia wafanyabiashara hawa
wadogo wadogo kusogea mbale zaidi na kuelimika ambapo wakielimika kutakuwepo na ongezeko la dhamani.
Aidha wamesema kuwa kwa sasa ivi wameamaa
kuwatafuta na kufanya kazi nao ili kuweza kuwasaidia kutangaza bidhaa zao
ambazo zinatengenezwa hapa nyumbani.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia