AJTC BINGWA WA BONANZA LA TISA LA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA KASKAZINI
Posted by
woinde
on
Monday, June 30, 2014
in
MATUKIO
MICHEZO
|
|
mwenyekiti wa Taswa Taifa Juma Pinto akiwa akiwa anakagua timu ya mpira wa pete kutoka AJTC kabla ya mechi ya fainaili kuchezwa |
|
washabiki wa timu ya AJTC wakiwa wanashangilia mara baada yakukabidhiwa kombe katika bonanza la Taswa |
Meneja
masoko wa Mega trade, Godluck Kway akitoa neno ndani ya bonanza hilo
Mkuu
wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL
akiongozana na meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Mega Trade
Investment Godluck Kway kukagua timu ya netball ya chuo cha uandishi wa
habari AJTC
kikosi cha timu ya mpira wa miguu kutoka cho cha AJTC
Nahodha
wa timu ya mpira wa miguu wa AJTC Bw. Alli Ahmedi akikabidhiwa kombe la
ubingwa na Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana
kutoka TBL
Timu za
Chuo Cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika
bonanza la tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, lililofanyika
uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Katika
bonanza hilo, ambalo mgeni rasmi alikuwa, Mwenyekiti wa Taswa Taifa,
Juma Pinto jumla ya timu 10 zilishiriki na liliandaliwa na Taswa
Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique.
Timu ya
soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4
timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo, waliwashinda timu
ya chuo cha uandishi wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli
18-5.
Mgeni rasmi
Pinto ambaye pia ni Mjumbe wa bodi vya Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro
alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa soka alipewa
kikombe, pamoja na fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.
Mshindi wa
pili wa soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa mpira wa pete alizawadiwa
kikombe na fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa pili akikabidhiwa tsh
50, 000.
Katika
bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, (TBL),
kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro,
Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel,
Timu
zilizoshiriki ni Radio 5, timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa
Manyara, Salam Club, IMS na Taswa Arusha ambayo iliibuka na ushindi
katika kukamata kuku.
Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi nzuri waliofanya.
“Nachukuwa fursa hii kuwapongeza sana Taswa Arusha kwa kuandaa bonanza hili kwani halifanyiki sehemu nyingine nchini”alisema
Awali
Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi TBL kuendelea kudhamini
bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi wa Arusha.
Meneja
masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza wanahabari kwa kushiriki
kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kuendelea kulidhamini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia