BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI ,WATANGAZAJI KUFANYIKA JUNE 28 KATIKA VIWANJA VYA GENERA


Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa Juma,

Bonanza  la waandishi wa habari na watangazaji Kanda ya Kaskazini linatarajiwa kufanyika june 28 katika viwanja vya General tyre  jijini Arusha na kushirikisha zaidi na wanahabari 150 na wadau wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa Juma, alisema maandalizi muhimu ya Bonanza yameanza.

Juma alisema bonanza hilo,ambalo huandaliwa na TASWA Arusha na kampuni ya MS UniquePromotion litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari mkoa wa Arusha,  ambayo itashirikisha baadhi ya wajumbe wa kamati ya tendaji ya TASWA Taifa.

Hata hivyo alisema bado TASWA Arusha na kampuni ya MS Unique wanatafuta wadhamini wa bonanza hilo ambalo litakuwa ni la tisa kufanyika.

Juma alisema hivi karibuni wadhamini wa bonanza hilo, watatangazwa sambamba na zawadi kwa washindi.

Alisema katika tamasha hilo, wanahabari na wadau wa habari watashiriki katika michezo ya soka, kuvuta kamba, mbio za magunia,mpira wa pete, kukimbiza kuku na kucheza muziki.

Katika tamasha la mwaka jana, hakukuwa na bingwa wa soka baada ya TASWA Dar es Salaam na timu ya chuo cha Uandishi wa habari(AJTC) kushindwa kufungana.

Kwa upande wa mpira wa pete TASWA Dar es Salaam, alishinda, huku katika mchezo wa kukimbiza kuku TASWA Arusha ilishinda na katika kamba timu ya Sunrise ilishinda wakati timu ya radio 5 na Arusha one zilitamba katika mbio za magunia.
Timu ya Waandishi na watangazaji toka mkoa wa Manyara ya ORS ilishinda zawadi ya timu yenye nidhamu,timu nyingine zilizoshiriki ni Wazee Klabu,Pespi,TBL na timu ya timu ya Kitambi noma.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post