Mwenyekiti na mwasisi wa kikundi cha kujitolea kinachowalea watoto wenye mfanano wa kikundi cha Trabajo Voluntario, Marisa Yussuf Himid akionyesha bango wakati maandalizi ya shughuli hiyo.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
ZAIDI ya watoto mfanano 50 na familia zao wanatarajiwa kujumuika na watu wengine katika viwanja vya Ngome Kongwe kwa mashamushamu ya kuonesha upendo na kushuhudia mateso yanayowapata watoto hao.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya kujitolea ya mjini Zanzibar ya Trabajo Voluntario, (Voluntary Work) inakutanisha watoto hao wakishirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya tamasha la filamu la kimataifa la Zanzibar (ZIFF).
Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa wa Trabajo Voluntario, Marissa Himid Yusuf taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005 ili kusaidia watoto mfanano, lengo lao kubwa la kuwakusanya hapo ni kuwaonesha upendo na pia kujadili maslahi yao.
Alisema kwa sasa watoto wengi wenye hali ya ufanano hawatimiziwi haki zao msingi ikiwemo ulinzi na wala hakuna sera inayohakikisha kwamba wanalindwa na wanapewa haki nyingine kama watoto wengine hasa elimu itakayowawezesha kuwa na kitu cha kufanya katika maihs ayao.
Alisema katika maelezo yake kwamba kuna simulizi za kutisha kuhusu watoto hao na kwamba wapo baadhi ya wanwake wapo tayari kutoa nushuhuda wa yaliyotokea katika famulia zao baada ya watoto walionao kubainika kwamba wana tatizo la mfanano.
Alisema pamoja na ushuhuda huo mkusanyiko huo umelenga pia kukemea maovu wanayofanyiwa watoto hao na watu wazima kwamkusanyiko huo ni kuelimishana kuhusu watoto hao na kuhimiza ushiriki wa serikali na jamii kuhakikisha usalama wao na kupata haki yao ya msingi ya kupendwa na kulindwa.
Alisema pamoja na kuwapo kwa haja ya sera zinazotekelezeka ili kutoa ulinzi kwa watoto na familia zao, ipo haja kw ajumuia kuondoa unyanyapaa dhidi yao.
Kwa kusanyiko hilo la Ijumaa tunategemea wananchi watakuja kujifunza kuondokana na unyanyapaa na pia kufanya kampeni ya kuondoa hali hiyo miongoni mwa jamii.
Marisa Yussuf Himid, ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya TrabajoVoluntario, alisema mamlaka zinaozhusika zinaonekana kukimbia jukumu la kulea watoto hao ambao wana manufaa makubwa katika jamii wakielekezwa na kujua.
Aidha alitumia wasaa kuiomba serikali na mamlaka zake kuangalia suala la kunyan yaswa kwa watoto hawa, kufuatilia na kuwafikisha kizimbani wale wote wanaowatesa watoto hao kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwabaka, kuwanajisi na hata kuwalawiti.
Aidha ametaka shule kutumika kufunza watoto hawa ambao elimu yao huchukua muda mrefu.
Kwa mujibu wa Marissa mgeni rasmi atakuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya ulemevu, AbedaAbdallah Rashid, ambaye atazungumza.
Aidha balozi wa watoto mfanano Fareed Kubanda, atazungumza wakati wa kufunga kusanyiko hilo.