Sakata
la Michael Wambura kuondolewa kwenye kinyang’anyiro za uchaguzi wa mkuu
wa Uraisi wa klabu ya Simba SC leo limefikia tamati.
Kamati ya rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF, imetengeu
maamuzi ya kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba SC wa kuliengua jina la
mgombea wa Urais wa klabu hiyo, Micheal Richard Wambura.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, wakili Julius Mutabazi Lugaziya amesema
mchana huu katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa TFF, jijini Dar es salaam kuwa kamati yake ilikaa juzi na
jana na kufikia maamuzi ya kutengua maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya
Simba chini ya mwanasheria, Dkt. Damas Ndumbaro kwasababu klabu hiyo
ilikiuka kanuni ilijiwekea yenyewe kwa mujibu wa katiba.
Lugaziya amesema kuwa uamuzi wa kumrudisha Wambura umeangali zaidi
busara kwasababu Simba ilikiuka katiba yake kwa kumuacha mwanachama
aliyesimamishwa kuendelea kufanya shughuli za klabu, na kama akiondolewa
basi katiba na kamati ya uchaguzi vyote vitakuwa batili.
“Tangu aliposimamishwa, muomba rufani (Wambura) hajawahi kuchukuliwa
kama mtu aliyesimamishwa. Kwanini?, kupoteza haki za uanachama ni pamoja
na kupoteza haki za kulipa ada, haki za kushiriki mikutano, haki ya
vikao vya maamuzi na haki ya kuteuliwa katika vyomvyo mbalimbali vya
Simba SC”. Alisema Wakili Lugaziya.
“Tangu kutangazwa kusimamishwa, amekuwa akishiriki shughuli za Simba.
Amekuwa akishiriki mikutano yote mikuu na dhararu, ikumbukwe kuwa
mwanachama halali tu ndiye anatakiwa kushiriki mikutano hiyo na
mwanachama ambaye amesimamishwa hatakiwi kushiriki, lakini tangu
kutangaza kusimamishwa, Wambura amekuwa akishiriki”. Alifafanua
Lugaziya.
“Kubwa zaidi, mpaka sasa Wambura ni mjumbe wa kuteuliwa wa kamati ya
utendaji ya Simba na alishiriki katika mikutano ya katiba pamoja na
kushiriki kuiteua kamati ya uchaguzi”. Wakili huo aliongeza kuwa kama
mtu batili ameshiriki kufanya maamuzi, basi maamuzi nayo ni batili.
“Wambura alishiriki katika mkutano wa katiba na kuiteua kamati ya
uchaguzi, maana yake kama Wambura ni batili, basi katiba na kamati ni
batili”. Kama tunafikia maamuzi ya kusema katiba na kamati ya uchaguzi
ya Simba si halali, kwasababu mtu batili alishiriki, athari yake ni
kubwa. Kamati alishasema huko nyuma kwamba Simba ilikuwa inamchukulia
Wambura kama mwanachama”. Alisema Lugaziya.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia