mzee
wa kanisa la Waadventista wasabato mtaa
wa kijenge Agrey Tumaini akiwa anagawa maindi kwa wananchi wa kitongoji cha nyamagana
Zaidi ya wananchi
50 wa kitongoji cha Nyamagana
kilichopo katika kijiji cha Themi ya simba wilayani Arumeru MKoani
Arusha ambao waliathiriwa na mafuriko yaliotokea mwisho mwa mwezi wa nne mwaka
huu wamepatiwa msaada wa chakula na nguo kijijini hapa.
Akikabidhi chakula
hicho mzee wa kanisa la Waadventista wasabato
mtaa wa kijenge Agrey Tumaini
alisema kuwa wameamua kuwasaidia wananchi hawa kutokana na janga ambalo
liliwakuta la kuingiliwa na mafuriko ya maji
ambapo yaliwasababishia nyumba pamoja na mazao yao kuezuliwa na maji
hayo
Alisema kuwa wao kama kikundi cha WAMO kutoka katika kanisa hilo waliguswa sana na
tatizo hili ambalo liliwatokea hivyo wakaamua kujichanga na kununua vyakula
ivyo na nguo kwa ajili ya wahanga hao wa mafuriko.
Alisema kuwa wameweza kutoa gunia kumi za mahindi ,maharage kunia
tatu,unga wa ugali pamoja na nguo kwa ajili ya watoto wa wananchi ambao walikubwa na janga hilila
mafuriko.
“sisi tumeguswa sana na tukio hili wenzetu kukubwa na mafuriko kwa kweli wameadhirika vikubwa kwani
wengine awana sehemu zakukaa wengine walikuwa wamelima mazao yao kama mahindi
yaliezuliwa na mafuriko hayo yaani kiukweli hadi sasa kuna watu awajui
wataishije kwa mwaka huu lakini tumeona sio vibaya iwapo tukiwasaidia ichi
kidogo tulichonacho maana ata neno la
mungu linasema katika mathayo uwa
mlikuja na njaa nikawapa chakula,mlikuja uchi nikawavisha sasa na sisi tumeamua
kuwapa ichi kidogona tunawaomba watu wengine waendelee kujitokeza kwa wingi
kuwasaidia wananchi hawa kwani wapo katika mazingira magumu sana”alisema
Tumaini.
Akipokwa msaada huo mmoja wa wananchi hao alietambulika kwa
jina la Gidion Maganga alisema kuwa
anashukuru sana kanisa hili la wa sabato kwa kuja kuwasaidia kwani kuna baadhi
yao walikuwa hawajui hatima ya maisha yao kwani ata chakula kwao kupata ni tabu
..
Alisema kuwa pamoja kuwa kuna baadhi yaviongozi na taasisi
ambazo zimewapelekea chakula kama maindi ,magodoro pamoja na nguo lakini bado wanaitaji maada
kwani mvua zile ziliwachukulia vitu vyao vingi ikiwemo mazao maindi waliokuwa
wameyaifadhi ndani vyombo ,magodoro na sio ivyo tu lakini pia zileweza kumuua
mwananchi mmoja.
Akizungumzia tukio hilo mwananchi mungine ambaye aliyejitaja
kwa jina la Zainabu Minja alisema kuwa siku hiyo ya tukio lilitokea majira ya
saa saba usiku wakati wamelala huku mvua
ikinyesha ndipo gafla waliona maji mengi yamekuja na kujaa ndani ya nyumba
kitu ambacho kiliwaogopesha zaidi ni pa le maji yale yalivyoanza kusomba
vitu.
“yaani ndugu muandishi usione apa yaani maji yalikuja na
kasi unaona hii chuma ina uzitowa kilomia ndio niliichukuwa nikaishika na uyu
ni mama yangu na unamuona alivyo mzee nilimwambia ashikilie iyo chuma akashika
mwishowe mikono ikafa ganzi ndipo nikachukua kanga na kumfunga kiunoni
nikaunganisha na chuma ili asipelekwe na maji ila nashukuru mungu alituona
pamoja vitu vilizolewa lakini sisi ni wazima kwakweli”alisema bi Zainabu
Alitoa wito kwa wananchi serekali pamoja na taasisi
mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuwasiaidia kwani wapo katika halingumu
sana katika kipindi hichi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia