SUAREZ NA MAJANGA YAKE KOMBE LA DUNIA

KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Mshambuliaji matata wa timu ya soka ya Uruguay Luis Suarez anakabiliwa na marufuku ya mda mrefu itakayomlazimu kukosa mechi nyengine za michuano ya kombe la dunia iwapo atapatikana na hatia ya kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.
Mchezaji wa Italy Chiellini akionyesha jeraha alilopata baada ya kung'atwa na Suarez.
Mchezaji wa Italy Chiellini akionyesha jeraha alilopata baada ya kung'atwa na Suarez
Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha harakati za kumuadhibu mcheza huyo kufuatia ushindi wa moja kwa bila dhidi ya Italy siku ya Jumanne.
Chiellini amedai kwamba Suarez alimng'ata bega lake licha ya Suarez kudai kuwa ni mchazaji huyo aliyemchezea vibaya.
SUARES NA CHIELLINI.
Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akapigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi 24 ama miaka miwili.
Refa aliyesimamia mechi hiyo kutoka Mexico Marco Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kisa hicho, lakini FIFA bado inaweza kumuadhibu Suarez.
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Liverpool Jan Molby anatarajia kwamba Suarez atapigwa marufuku kwa mechi zote za kombe hilo zilizosalia.
Raia huyo wa Denmark ameliambia gazeti la Liverpool la Echo kwamba '' nina hakika FIFA itachukua swala hilo la Suarez kama mfano kwa wengine''.

''Ni dhahiri kwamba matumaini yake ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia iliosalia yamekwisha na ninataraji kwamba FIFA itampatia marufuku ya mda mrefu''
Kuchezewa vibaya pamoja na nguvu kutumika isivyo vyote mchezaji machachari Luis Suarez alikumbana navyo kwenye mchezo huo. 
Na hata yule aliyemng'ata, alimchezea madhambi mengi.
Hata hivyo mara baada ya mchezo Suarez alionekana mchangamfu...na wala asiyeonekana  kujutia kwa lililotokea.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post